Mtoto a Usher Raymond mwenye miaka 5 awahishwa hospitali kitengo cha
watu mahututi (ICU) baada ya kunusurika kuzama ndani ya pool la
kuogelea. Raymond V alikuwa na shangazi yake ndani ya pool lililopo
nyumbani pale alipokwama katika tundu la pool hiyo alipokuwa akijaribu
kufata toy.
Shangazi huyo na mfanya kazi walishindwa kutoa mkono wa mtoto huyo uliokuwa umenasa katika tundu hilo na kuanza kupiga makelele.
wafanyakazi waliokuwa akishughulikia audio na visual katika nyumba hiyo
walikimbia na kujirusha kwenye pool na kumuokoa mtoto huyo ambapo
iliwalazimu kumfanyia CPR (kumkandamiza kifuani) na hatimae kufanikiwa
kumzindua.
Raymond V aliwahishwa hospitali ambapo anasemekana kuurudi katika hali
yake ya ufahamu na anaendelea vizuri, Usher Raymond hakuwepo nyumbani
kwake wakati tukio linatokea
Raymond V ni mdogo wa watoto wawili wa Usher na mkewe wa zamani, Tameka
Raymond, na alikabidhiwa na kupewa ruhusa ya kuwaangalia watoto wake
Agosti 2012, baada ya kutalakiana na mkewe huyo.
Mke huyo wa zamani wa Usher amepeleka hati za kisheria kuomba dharura ya
kusikilizwa haraka wiki hii katika jitihada za kururudishiwa watoto
wake baada ya baba yao kushindwa majukumu yake kama baba na kuwaachia
watu wengine kuwaangalia watoto wake.
Ajali ya jana imetokea ikiwa ni mwaka tu tangu mtoto wa kambo wa Usher
Kile Glover mwenye miaka 11 kufariki kwa ajali ya Jet Ski akiwa katika
ziwa Lanier, Georgia.
EmoticonEmoticon