Internet jana
ilichemka kwa moto aliouanzisha Kendrick Lamar kwenye wimbo
alioshirikishwa na Big Sean, Control ambapo pamoja na kuwataja rappers
kibao kuwa atahakikisha anawapoteza wote kwenye ramani, alijipa cheo cha
Mfalme wa New York.
Meek Mill ambaye alitajwa pia amejibu lakini amesema alichokiongea Lamar si tusi na wala hawezi kutoa ngoma ya kumdiss.
“Ni hakika hakutukana. Kendrick Lamar,sidhani kama alikuwa anajaribu
kututukana. Wote tunafahamiana vizuri.Kuna majina mengi yaliyotajwa.
Napenda game za aina hiyo. Sidhani kama ametukana. Ni kitu cha
ushindani. Naishi kwa ushindani. Kila mtu anayenifahamu anajua kuwa huwa
sikubali kushindwa. Sitatoa wimbo wa kumdiss Kendrick Lamar. Lakini
kama anataka kushindana, tutaenda kufurahi,” alisema Meek Mill.
EmoticonEmoticon