KICHANGA CHAZALIWA NA JINSIA MBILI

 
Mganga mfawidhi wa Hospitali ta Wilaya ya Tunduru Dkt. Joseph Ng'ombo akimuangalia mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana macho, pua na Shavu linalo shika mdomo wa juu, kushoto ni mkunga wa zamu katika Hospital hiyo Rukia Nguo akiwa akiwa amekishika kichanga
Huu ndiyo muunekano wa kichanga hiki usoni.

Mkono wa mkunga huyo ukionyesha maungo ya kichanga hicho kilichozaliwa kikiwa na sehemu nyeti mbili ikiwepo ya kiume kwa juu na ya kike kwa chini.
----------------------------------------------
Na Steven Augustino, Tunduru
MAJONZI na Simanzi zilitawala kwa wanafamilia na Wauguzi katika hosipitali ya Wilaya ya Tunduru baada ya ndugu yao mkazi wa Kijiji cha Kadewele Mjini hapa aliyetambuliwa kwa jina la Rehema Safi (42) kujifungua Mtoto wa ajabu mbaye pamoja miongoni mwa maajabu hayo nipamoja na kuzaliwa akiwa na Jinsia Mbili.

Aidha Kichanga hicho ambacho kimezaliwa kikiwa na uzito wa kilo 1.8 pia kimezaliwa kikiwa hakina Pua,macho na Shavu ambalo hushikilia mdomo wa juu.  

Tukio hilo ambalo lilisababisha mshtuko na taaharuki kwa wataalamu wanaotoa huduma ya kiafya limetokea katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Agosti 5 mwaka huu.

Mkunga wa zamu katika Wodi ya wazazi iliyopo katika hospitali hiyo Rukia Nguo alisema kuwa pamoja na uzowefu wake wa muda mrefu katika kada hiyo hajawahi kuona kiumbe cha aina hiyo.

Alisema baada ya tukio alilazimika kuwaita waganga na wauguzi wenzake ili wamsaidie kutazama kichanga hicho ili kujiridhisha juu ya tukio hilo akidai kuwa awali akiwa peke yake akishindwa kukitambua kiumbe hicho kama ni binabamu ama la ingawa kilionekana kuwa na viungo vingine vya kibinadamu.

Kufuatia hali hiyo Mkunga huyo akatoa wito kwa wanawake wenzake kuachana na tabia ya kutumia dawa za kienyeji na badala yake waende hospital kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa tabibu.
“unajua sisi wanawake wengi tumekuwa na tabia ya kuchukua na kuanza kuzitumia dawa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki “ alisema Nguo na kuongeza kuwa matumizi ya dawa za aina hiyo zinaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo yanayo sababisha kuzaliwa kwa watoto wenye upungufu wa viungo.    

Akizungumza kwa unyonge juu ya tukio hilo mama mzazi wa Mtoto hoyo ambaye hadi sasa hajapatiwa jina, Reheme Safi ambaye uzazi huo ni wa tano alisema kuwa hana budi kulipokea tukio hilo kama changamoto ya maisha kwani mtoaji nimungu na kwa hatua hiyo hawezi kubishana na uumbaji huo.

  ukilinganisha na tukio la Kutunza mimba ya Mtoto kwa Miezi 9 huku ukiwa na matumaini ya kupata mtoto atakaye kusaidia maishani,sijisikii vizuri kupata Mtoto wa aina hii lakini sinanjia ya kuyabadilisha matokeo hayo “ alisema Reheme na kuongeza kuwa yeye anamuachia mungu juu uumbaji huo.

Akizungumzia histolia ya jinsi ulivyo patikana ujauzito huo alisema kuwa kwanza yeye hakutarajia kuupata kwavile kwa zaidi ya miaka miwli alikuwa akitumia Dawa za uzazi wa Mpango aina ya (DEPO PROVELA) ya sindano ambayo wanawake wengi wanaopanga uzazi huitumia kwa kuchoma sindao moja kila baada ya miezi mitatu.

Alisema akiwa katika hali hiyo ghafla alishangaa kuona tumbo lake linakuwa zito na baadae kitu kikaanza kucheza tumboni na alipokwenda hospitali na kupimwa alishangaa kuelezwa kuwa huo ni ujauzito na kinachocheza ni Mtoto.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya serikali ya Wilaya ya Dkt. Joseph Ng’omboa amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa maafisa tabibu wanaendelea kufanya utafiti wa chanzo cha tukio hilo kwa kumpima mama huyo kama ana magonjwa ya kuambukiza ama la.

Alisema mtoto kuzaliwa akiwa katika hali hiyo kunaweza kusababishwa na mambo mengi yakiwemo magonjwa ya zinaa, kukosekana kwa virutubisho Fulani wakati wa uumbwaji wa viungo mwilini ama mama mzazi kutumia madawa wakati akiwa na mimba changa.

Aidha Dkt. Ng’ombo pia akatumia nafasi hiyo kuwahamasisha akina mama wajawazito kuhudhulia Kliniki katika kipindi chote baada ya kupata ujauzito na kwenda kujifungulia hospitali kwa ajili ya kupata msaada wa maafisa tabibu wakati wote. 
Previous
Next Post »