Meneja
wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya
mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila akizungumza juu
ya umuhimu wa mtandao huo wakati wa kutoa msaada kwa watoto yatima
kituo cha Amani Nsagala Uyole.
Baadhi ya watoto katika kituo cha Kulelea yatima cha Aman Nsagala uyole wakimsikiliza kwa makini Meneja
wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya
mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila
Mmoja ya wananchi waliokiuja kushuhudia kutolewa kwa Msaada huo , akiuliza swali juu ya Tovuti hiyo.
Baadhi ya watoto katika kituo cha watoto yatima cha Aman Nsagala wakiimba Nyimbo kabla ya kukabidhiwa msaada huo.
Meneja
wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya
mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila kushoto
akikabidhi msaada wenye thamani ya Tsh 1,500,000 katika kituo kituo cha
kulelea watoto yatima cha Amani
Hili ni eneo ambalo watoto hawa hukutania na kujifunza mambo kadha wa kadha
Msimamizi
Msaidizi wa Kituo hicho kilicho chini ya Idara ya Wanawake ya Kanisa la
Moraviani, Isabela Haonga akitoa neno la Shukurani kwa kampuni ya
LAJANN E-SYSTEM ENTERPRISES kwa msaada uliotolewa kwa watoto yatima
Meneja
wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya
mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila akiwa katika
picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Aman Nsagala Uyole.
JAMII
imetakiwa kuisaidia Serikali katika kuifichua na kuziba mianya
inayosababisha Watoto wa mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu
kuzidiu kuongezeka licha ya Asasi nyingi kujitokeza kuwahudumia.
Mwito
huo ulitolewa wa na Katibu Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi la Kanisa
la Moraviani Tanzania, Mchungaji Willy Mwasile, wakati akipokea msaada
kutoka kwa kampuni ya LAJANN E- System Enteprises ya Jijini Dar Es
Salaam kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto Yatima cha Aman Nsalaga
kilichopo Uyole Jijii Mbeya.
Mchungaji
Mwasile alisema ni vema utafiti ukafanyika ili kubaini chanzo cha
ongezeko la Yatima mitaani ili liweze kudhibitiwa na kuondolewa kabisa
kwa kudhibiti ndoa zisizo halali kwa wale wanaobeba mimba kiholela na
kutokuwa na uwezo wa kulea.
Akitoa
msaada huo Meneja wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kurusha
matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao
huu www.ligikuu.co.tz ,
Nzowa Wawila, alisema kutokana na kukaribia kufunguliwa kwqa pazia la
Ligi kuu wameona ni vema wakatoa msaada kwa jamii ili kutambua umuhimu
wao.
Alisema
kampuni yao inayofadhiliwa na Benki ya Banc ABC imeona siyo vizuri
misaada yote ikaishia Dar Es Salaam pekee ili hali kunawahitaji wengi
mikoani na ndiyo maana wakafika katika kituo cha Amani Nsalaga na kutoa
msaada.
Alivitaja
vitu vilivyotolewa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni Moja na Nusu(
1,500,000/=) zikiwa ni kwa ajili ya Mchele debe 10, maharage debe 5,
Sukari katoni 2 sabuni, kalamu chumvi na vifaa vya shule.
Aliongeza
kuwa kampuni yao inahusika zaidi na michezo na kwamba katika zawadi
ambazo walipaswa kuzitoa ilikuwa ni vifaa vya michezo lakii wameshindwa
kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya kituo kwamba watoto wanatakiwa
kula na kusoma hivyo vifaa vya michezo vitatolewa hapo baadaye.
Kwa
upande wake Msimamizi Msaidizi wa Kituo hicho kilicho chini ya Idara ya
Wanawake ya Kanisa la Moraviani, Isabela Haonga, akishgukuru kwqa niaba
ya watoto alisema msaada huo utasaidia kuboresha maisha ya watoto
kutokana na wengi wao kulelewa katika mazingira magumu.
Alisema
kituo hicho kinahudumia zaidi ya watoto 200 kwa kuwatafutia sare za
shule, ada na mahitaji yote ya shule, kuwajenga kisaikolojia, kuwakatia
bima za Afya pamoja na chakula hali inayosababisha Kitengo hicho
kushindwa kumudu gharama zote na kuomba msaada kwa wasamaria wema
wengine kujitokeza kutoa msaada.
EmoticonEmoticon