Jiji la Johannesburg
limemuomba radhi Mzee Nelson Mandela baada ya kutumiwa kimakosa onyo
kuwa huduma za maji na umeme zitakatwa.
Mamlaka za manispaa zimedai kuwa notice hiyo ilitumwa kimakosa kwa
mpigania uhuru huyo aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
Notice hiyo ilikuwa inataka alipe bili ya 6,468.48 ambayo ilipaswa
iende kwenye nyumba tofauti. Mandela mwenye miaka 95, bado yupo
hospitali jijini Pretoria alikokaa kwa miezi miwili.
EmoticonEmoticon