Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki Mhe.
Samuel Sitta akiwahutubia vijana (hawapo pichani) waliohudhuria wakati
wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililofanyika jana
jijini Dar es Salaam.
Bw.
Julius Toneshe aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Michezo akiongea wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la
Katiba jana jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Lenin Kazoba
(kushoto) akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta ( kulia) wakati wa
ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam.
Meneja
Mipango wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Bi. Rahma Bajun
akiongea baada ya kumkaribisha mgeni rasmi Mhe. Samuel Sitta kwa ajili
ya kutoa hotuba yake na kufanya ufunguzi rasmi wa Baraza la vijana la
Taifa la Katiba jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Taasisi ya Vijana ya Tanzania Youth Coalition Rebecca Gyum akiongea
wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba
lililofunguliwa rasmi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Samuel Sitta.
Baadhi
ya washiriki ambao ni vijana mbalimbali kutoka Wilaya 50 za mikoa yote
Tanzania wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Mhe. Samuel Sitta (hayupo
pichani) wakati akitoa hotuba kwa vijana hao. Salaam.
Picha
ya pamoja katikati ni Waziri wa Ushirkiano wa Afrika Mashariki Mhe.
Samuel Sitta, kushoto kwake ni Bw. Julius Toneshe na Meneja Mipango wa
TYC Bi. Rahma Bajun. Wa kwanza kutoka kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi
wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Lenin Kazoba na Meneja wa
Restless Development. (picha zote na Benedict Liwenga-Maelezo).
Waziri
wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashiriki Mhe. Samuel Sitta
amewaasa vijana kutoa maoni yao juu ya uundwaji wa Katiba mpya ambayo
haijengi mifumno ya serikali ya Udikteta, ubinafsi na ambayo
haitaibebesha mzigo Serikali.
Mh.
Sitta amesema hayo akifungua rasmi Baraza la Vijana la Taifa la Katiba
lililoandaliwa na Taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition (TYC)
kwa kushirikiana na Restless Development-UNFPA na ILO, lililojumuisha
vijana 120 kutoka Wilaya 50 za mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani na
ambao wanatoka katika mashirika mbalimbali, asasi, jumuiya na vikundi
mbalimbali vya vijana.
Waziri
Sitta amewaasa vijana kuwa TYC pamoja na vijana wengine nchini
wanalojukumu kubwa la mapambano dhidi ya kupinga ulafi katika mambo ya
uongozi, udikteta pamoja na ubinafsi kwani vinailetea mzigo serikali.
Ameongeza
kuwa vijana nchini wanatakiwa wawe Wanaharakati katika kujali maadili
mema na kusimamia kwa dhati pamoja na kupigania haki na usawa nchini.
Aidha,
kwa upande mwingine Waziri Sitta amevishukuru vyombo vya habari kwa
mchango wake mkubwa wa kufanya kazi ya kuhabarisha umma na pia
ameipongeza taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Coalition kwa kuandaa
baraza hilo kwa vijana wenzao, kwani litawasaidia kutambiua mambo ya
msingi yanayohitajika kuwepo katika Katiba mpya ya nchi.
Waziri
Sitta amesema kuwa katika kutoa maoni juu ya Katiba mpya, vijana
wanaweza kupata katiba yenye manufaa mazuri au yenye athari kwa maisha
yao, hivyo amewaasa vijana wote watumie fursa wanazozipata kupitia
baraza hilo lililoandaliwa na TYC, ili waweze kusikika katika mambo
yanayohitajika katika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taasisi
ya vijana ya Tanzania Youth Coalition ni moja ya taasisi iliyoundwa kwa
malengo ya kuhakikisha kuwa vijana wanashiriki na kushirikishwa katika
mchakato wa kuunda katiba mpya ulioanza mwaka jana hapa nchini.
EmoticonEmoticon