Waziri
mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa
ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri
mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la heshima la
vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya kuwasili nchini
Tanzania leo.
Gwaride
la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa
kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra
(kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es
salaam.
Waziri
mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma
akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri
mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya
kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
Waziri
mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano wa pamoja
na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na
Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck
Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya
makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za
uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika
sekta ya Nishati na Madini.
EmoticonEmoticon