TRENI YAMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI



“PRESS RELEASE” TAREHE 04. 07. 2013.

 

WILAYA YA MBEYA – AJALI YA GARI MOSHI [TRENI] KUMGONGA MTEMBEA KWA  

                                        MIGUU NA KUSABABISHA KIFO

 

MNAMO TAREHE 03.07.2013 MAJIRA YA SAA 12:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA NANENANE DARAJANI JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI MOSHI [TRENI] NAMBA 612 MALI YA TAZARA LIILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA YOHANA S/O MANGORANI NA HANSI S/O AMANYISYE LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA TUNDUMA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE JINSIA MWANAUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 20-25 ALIYEKUWA AMEKAA RELINI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. CHANZO KINACHUNGUZWA INGAWA TAARIFA ZA AWALI ZINADAI MAREHEMU ALIKUWA NA MATATIZO YA AKILI.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA UANGALIZI WA KARIBU NA WATU WENYE MATATIZO YA AKILI IKIWA NI PAMOJA NA KUWA MAKINI NA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

 

 

WILAYA YA MBEYA MJINI – JALADA LA UCHUNGUZI

 

MNAMO TAREHE 03.07.2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO ENEO LA SOWETO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO MAALUM WALIWAKAMATA 1. MWENZE S/O KAYUMBA, MIAKA 29, KYUSA, MFANYABIASHARA MKAZI WA SOWETO 2. ALBERT S/O MOMBA, MIAKA 38, MSAFWA, MFANYABIASHARA MKAZI WA SOWETO 3. FRED S/O PROTAS, MIAKA 18, MCHAGA, MKAZI WA MAMA JOHN NA 4. PETER S/O MWALA,MIAKA 19,MMALILA MKAZI WA SOWETO WAKIWA NA KARATASI ZA KUTENGENEZEA NOTI BANDIA ZAIDI YA 1,000 NDANI YA GARI T.337 AKV AINA YA TOYOTA COROLA WAKIWARUBUNI WATU KUWA WANATENGENEZA NOTI . WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA VIELELEZO TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAIMU  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI  ANATOA WITO KWA  JAMII KUACHA TAMAA YA UTAJIRI WA HARAKA  YA KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA ZISIZO HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

 

 

WILAYA YA MBOZI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

 

MNAMO TAREHE 03.07.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA MLOWO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA TUMAINI S/O ULIKWA, MIAKA 32,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA MLOWO  AKIWA NA  WENZAKE 4 WAKINYWA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] YENYE UJAZO WA LITA TATU [03] . MBINU NI KUNYWA POMBE HIYO WAKIWA WAMEJIFICHA KWENYE PAGALA. WATUHUMIWA NI WANYWAJI WA POMBE HIYO TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA SAMBAMBA NA KUWA HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

 

 

Signed By,

[BARAKAEL MASAKI   - ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »