TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI


“PRESS RELEASE” TAREHE 31. 07. 2013.

WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA MOTO

MNAMO TAREHE 30/07/2013 MAJIRA YA SAA 20:30HRS – HUKO SOKOMATOLA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASHA D/O ABDALLA, MIAKA 90, MHEHE, MKULIMA NA MKAZI WA SOKOMATOLA ALIUNGULIWA NYUMBA YAKE NA KUSABABISHA HASARA YA KUUNGUA KWA PAA LA NYUMBA YAKE, MADIRISHA PAMOJA NA VITU VILIVYOKUWA NDANI AMBAVYO THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA. CHANZO CHA MOTO HUO INADHANIWA KUWA NI HITILAFU ZA UMEME. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA NA TAHADHARI NA MAJANGA YA  MOTO ILI KUEPUKANA NA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA NA MIRUNGI

MNAMO TAREHE 30/07/2013 MAJIRA YA  SAA 22:00HRS HUKO ITEWE  JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA NTOKAMBALI S/O SINGINALI, MIAKA 27, MSAFWA, NA MKAZI WA ITEWE  AKIWA NA MIRUNGI  KG. MOJA NA NUSU [1.5] NDANI YA MFUKO MWEUSI WA RAMBO. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA MIRUNGI HIYO AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAANDALIWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


WILAYA YA MBEYA – KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 30/07/2013 MAJIRA SAA 02:30HRS NSONGWI JUU JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MAULID S/O CHARLES,MIAKA 25, MSAFWA, NA MKAZI WA UYOLE AKIWA NA BHANGI  ROBO KILO [¼] NDANI YA  MFUKO MWEUSI WA RAMBO . MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO AMEKAMATWA NA TARATIBU ZINAANDALIWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.



Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Previous
Next Post »