HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 27. 07.2013.
WILAYA YA MBEYA - AJALI YA GARI KUGONGANA NA MWENDESHAPIKIPIKI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 26/07/2013 MAJIRA YA
SAA 15:00HRS. HUKO ENEO LA KARNIVO MAFIATI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA JIJI NA MKOA
WA MBEYA. GARI NO T.666 BUK AINA YA VOX WAGEN POLO LIKIENDESHWA NA DEREVA IDDI
S/O SELEMANI, MIAKA 36, MMWELA, NA MKAZI WA SAE MBEYA LILIGONGANA NA PIKIPIKI
NO T.796 CHA AINA YA T/BETTER ILIYOKUWA IKIENDESHWA
NA DEREVA BOAZ S/O MWAKALASYA, MIAKA 27, MNYAKYUSA, NA MKAZI WA ILEMI NA
KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA PIKIPIKI PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA, GARI PAMOJA NA
PIKIPIKI VIPO KITUONI . KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI
NA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA.
Imesainiwa na,
[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon