KAMA HUKUPATA NAFASI YA KUONA PICHA ZA HARUSI YA NATASHA WA BONGO MOVIE TAZAMA HAPA

Na Imelda Mtema
NANI amenuna? Hayawi… hayawi sasa yamekuwa!

Mwigizaji mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ hatimaye amefunga ndoa ya uzeeni akiwa na umri wa miaka 46.

Suzan Lewis ‘Natasha’ katika pozi na mumewe Alex Humba Lumila siku ya ndoa yao.
Tukio hilo lililopambwa na cherekochereko za kufa mtu, lilijiri…

Na Imelda Mtema
NANI amenuna? Hayawi… hayawi sasa yamekuwa!
Mwigizaji mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ hatimaye amefunga ndoa ya uzeeni akiwa na umri wa miaka 46.

Suzan Lewis ‘Natasha’ katika pozi na mumewe Alex Humba Lumila siku ya ndoa yao.
Tukio hilo lililopambwa na cherekochereko za kufa mtu, lilijiri Jumamosi ya Julai 20, 2013 ambalo lilianzia kwenye Kanisa la Mt. Joseph lililopo Posta, Dar ambapo Natasha alifunga ndoa na mwanaume aitwaye Alex Humba Lumila.
Baada ya ndoa hiyo kufungwa kanisani hapo, mnuso ulihamia kwenye Ukumbi wa Magereza uliopo Ukonga, Dar.

...Wanandoa hao wakipozi na ndugu pamoja na jamaa.
Wakiwa ukumbini, mastaa wa Kibongo na wageni waalikwa waligonga ‘mpunga’  na vinywaji vya kila aina ambavyo vilikuwa vya kumwaga.
Gazeti hili lilipata nafasi ya kuzungumza na Natasha baada ya kufunga ndoa ambapo alisema kuwa siku hizi uzee unaishia Chalinze
kama unaelekea Dar na anachojua yeye ni kuwa hajawahi kuolewa na hiyo ndiyo ndoa yake ya kwanza.

Source :Global publisher
Previous
Next Post »