Japan wagundua tiba ya uso kwa kutumia konokono.

snail facial eewww

Saluni ya urembo huko Tokyo inatoa huduma ya kutibu ngozi ya uso kwa kutumia konokono.

Mtaalamu anayetoa huduma hiyo anadai kuwa ute wa konokono hao huondoa ukavu wa ngozi, kuondoa ngozi iliyokufa na kufanya uso uwe mng’aavu na laini kupindukia.Ute wa konokono hao una mchanganyiko wa proteins, antioxidants and hyaluronic acid ambazo huzuia uso kuzeeka.

Tiba hii hudumu kwa muda wa saa 1 ambapo mteja husafishwa uso na kukandwa kabla ya kuwekewa usoni konokono 5 wa salon hiyo.Huduma hii hutolewa kwa takribani dola 245, huwa inajumuishwa na masks na electrical pulse machine.


Previous
Next Post »