Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Simu ya Samsung, Sylivester
Manyara akiongea na simu na mmoja wa washindi wa mwezi Juni ambao ni
wateja walionunua bidhaa za kampuni hiyo hatimaye kuingia kwenye droo.
Washindi hao walipewa zawadi malimbali.
Dar
es Salaam. Kampuni ya SamSung maarufu kwa kuuza simu, imeamua
kuwasaidia wateja wake kwa kuwapa mbinu za kutambua simu bandia kabla ya
kutoa fedha wakati wa kununua.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo,
Sylvester Manyara alisema mbinu hiyo ni kuanzishwa kwa mfumo maalumu
unaoitwa E Warranty ambao una uwezo wa kuzisoma simu za kampuni hiyo
ambazo siyo bandia.
Manyara alisema mfumo wa E Warranty unawezesha
watumiaji wa simu za Samsung kutambua simu feki ambazo zipo sokoni
zikiwa na nembo ya kampuni hiyo.
‘’Kampuni ilibuni mfumo huo baada ya kuona zipo kampuni zilizoamua kutengeneza kwa kuigiza simu za .Samsung’’ alisema.
Alisema soka la simu kwa sasa linakabiliwa na
matatizo mengi yakiwamo ya kuenea kwa simu feki na ndiyo maana waliamua
kuwa na mfumo wa E Warranty ili kuwawezesha wateja wao kuepukana tatizo
hilo.
“Ili kujua kama simu ni halali, mtumiaji anatakiwa
kuandika kwenye ujumbe neno Check likifuatiwa na alama ya nyota kisha
namba ya ya simu iliyomo ndani karimu na herufi za ‘IMEI’ ikifuatiwa na
alama ya reli. Baada ya kufanya hivyo ujumbe huo autume kwenda katika
namba 15685 na baada ya ya muda atapa majibu yatakayokuwa yakielezea
hadhi ya simu hiyo ya Samsung,” alisema Manyara.
Katika hatua nyingine zaidi ya watumiaji 10 wa
simu za Samsung ambao wamejisajili kwenye mfumo huo wa E warant
walijipatia zawandi mbalimbali baada ya kuibuka washindi katika bahati
nasibu inayoendeshwa na kampuni kwa wateja wake waliojiunga na huduma
hiyo.
EmoticonEmoticon