Watoto
wawili wamekufa na mmoja wao kunusurika mauti, baada ya kuungua kwa
moto uliosababishwa na kibatari kilichounguza nyasi za kijumba
walichokuwemo. Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga amesema
ajali hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki jana katika mtaa wa Mitwero,
katika kata ya Rasbura ya Manispaa ya Lindi na kuwataja waliokufa kuwa
ni Maliki Kasimu (7) na na Selemani Fadhili (5) wakati aliyenusurika ni
Juma Abdallah.
Mzinga amesema watoto hao watatu waliofika kwa mzee mmoja wa jadi,
walikuwa wakijenga nyumba kwenye michezo yao wakati wakiwasubiri wenzao
wafike siku za usoni, tayari kwa shughuli ya jando. Siku ya tukio, moto
huo ulishika nyasi zilizokuwa ndani ya shimo na kuwaka na kuwachoma
Maliki na Selemani ambapo mwenzao, Juma alifanikiwa kukimbia na
kujiokoa. Wanakijiji wanasema mwangalizi wa jando hilo alikuwa mbali na
eneo la tukio na hivyo kushindwa kuwaokoa
EmoticonEmoticon