FUNKE : ASEMA NDOA KITU GANI?



MWIGIZAJI wa Nollywood ambaye huvutia wanaume wengi, Funke Adesiyan ameweka bayana kuwa kwa sasa hataki ndoa.Badala yake mwingizaji huyo aliyeyakuza matiti  yake amesema anachohitaji ni mwamamume wa kumridhisha kimapenzi na si kukurupukia ndoa.Ni mwigizaji mtata ambaye kauli zake mara nyingi hutengeneza vichwa vya habari.

“Ndoa ya nini? Ninachohitaji ni liwazo la aina yake katika mahaba. Ndoa wakati mwingine ni kero,” alisema Funke.Aliongeza: “Unaona matiti yangu? Haya ni ya kupandikiza na hapo ndipo ninapowazingua wanaume.“Kwa taarifa yako wanaume wengi katika dunia ya kisasa hupenda matiti makubwa.”

Kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwake kuwa anapenda kuvaa nguo zenye utata, Funke alisema hilo ni jambo binafsi.“Nadhani si mbaya kuheshimu uhuru wa mtu. Mavazi yangu sioni kama ni tatizo.”

Alisema kila siku anajaribu kuishi kulingana na mazingira ya Kiafrika lakini akiwa huru na si kulazimishwa na mtu nini cha kufanya.Anakula vyakula vya asili tofauti na waigizaji wengine maarufu.

“Kudharau asili yako ni dhambi kubwa na pia kufuata mkumbo wa kuolewa pia ni balaa…acha niishi nipendavyo.”
Previous
Next Post »