“PRESS RELEASE”
TAREHE 05. 07. 2013.
WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI - KUCHOMA NYUMBA MOTO.
MNAMO TAREHE 04.07.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA ILUNGU – IZIWA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI WALICHOMA MOTO NYUMBA YA MUSA S/O KEYA,MIAKA 35,MSAFWA,MKULIMA
,MKAZI WA IZIWA ILIYOJENGWA KWA MATOFALI MABICHI NA KUEZEKWA KWA KUTUMIA
NYASI NA KUTEKETEZA MALI ZOTE ZILIZOKUWA
NDANI YA NYUMBA HIYO. CHANZO NI TUHUMA ZA KISHIRIKINA BAADA YA WANANCHI
KUMTUHUMU KAKA WA MHANGA SAMSON S/O KEYA,MIAKA 60,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA
ILUNGU AMBAYE ALIKUWA AMEJIFICHA NDANI
YA NYUMBA HIYO KUWA NI MCHAWI NA AMEMLOGA MAREHEMU ESTER W/O MUSA MKE WA MHANGA
. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA KWANI SAMSON S/O KEYA ALIFANIKIWA
KUTOKA NDANI YA NYUMBA HIYO NA KUKIMBIA. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOTEKETEA
KWA MOTO BADO KUFAHAMIKA. KUFUATIA TUKIO
HILO WATU SABA WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO
AMBAO NI 1.YOHANA S/O SOLOMONI, MIAKA 38,MSAFWA,MKULIMA 2.TUMAINI S/O ANTHON,MIAKA 25,MSAFWA,MKULIMA 3.MOSHI S/O GEORGE,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA .4. DAUD S/O LINGI,MIAKA 25,MKULIMA,MSAFWA , 5.MUSA S/O PHILIPO,MIAKA 36,MSAFWA,MKULIMA ,6.TAMSON S/O GWILAJE,MIAKA 27,MSAFWA NA 7. LASTON S/O MBALAMWEZI,MIAKA 52,
MKULIMA ,MSAFWA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ILUNGU-IZIWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI
. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI
POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINARUDISHA NYUMA MAENDELEO. AIDHA ANATOA RAI KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA WATU
WENGINE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA
KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
WILAYA YA MBEYA - KUPATIKANA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
MNAMO TAREHE 04.07.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA
ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA EZEKIA S/O
ALFRED, MIAKA 34,KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA ILOLO AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] UJAZO WA LITA 8. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO YUPO MAHABUSU. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
Signed By,
[BARAKAEL MASAKI -
ACP]
KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon