TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI





“PRESS RELEASE” TAREHE 14. 06. 2013.




WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.


  MNAMO TAREHE 13.06.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO ENEO LA NZOVWE BARABARA YA MBEYA / TUNDUMA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI STJ 9619 AINA YA L/ROVER 110 MALI YA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA [TRA] MBEYA LIKIENDESHWA NA DEREVA HAKIM S/O MWALUPINDI,MIAKA 37,MMALILA,MKAZI WA MBALIZI LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GRACE D/O CHRISTOPHER AMBAYE ALIKUWA MJAMZITO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO . CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI PAMOJA NA MAGAZINE
                                          MOJA TUPU YA SMG.

 

MNAMO TAREHE 12.06.2013 MAJIRA YA SAA 08:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAMBI KATOTO WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIFANYA MSAKO  WA PAMOJA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA WANYAMAPORI [TANAPA] KUTOKA MKOANI IRINGA WALIMKAMATA MUSSA S/O YUSUPH,  MIAKA 35, MUHA, MKULIMA, MKAZI WA KAMBI KATOTO AKIWA NA NYARA ZA SERIKALI 1. MFUPA WA TEMBO 2. MKIA WA PALAHALA 3.  MGUU WA KWARE 4. MGUU WA FUNGO PAMOJA NA MAGAZINE MOJA TUPU YA SILAHA YA SMG. MBINU NI KUFANYA UPEKUZI NYUMBANI KWA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA NI JANGILI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI NYARA ZA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

 

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI.

 

MNAMO TAREHE 13.06.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO ENEO LA BLOCK Q SOWETO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA CHARLES S/O FRANCE, MIAKA 26, MSAFWA, MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILEMI AKIWA NA MISOKOTO 21 YA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 105. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
 

[ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »