Prezzo Ashtakiwa Kwa Unyanyasaji Na Utumiaji Wa Madawa

 


Rapper maarufu wa Kenya na msanii wa manzii kibao,Prezzo amekuwa mtalaka rasmi
Mahakama kuu ya Nairobi imeruhusu kesi ya talaka kusikilizwa baada ya mkewe Daisy Jematia Kiplagat(hayupo pichani) kumshtaki Prezzo na kuhalalishwa
Daisy alifungua kesi akiomba talaka mnamo mwaka 2012 dhidi ya Prezzo lakini Prezzo(Jackson Makini)hakujitetea
Jaji mkuu wa mahakama hiyo Luka Kimaru alikubaliana na kesi hiyo na kumwamuru Prezzo alipe gharama ya matumizi ya mtoto wao aliyezaliwa March 2009 kiasi cha Ksh.500,000
''Mshtaka na mshtakiwa wameachana kuanzia Nov 2011.Kutokana na sababu hapo juu,hii mahakama haina jinsi na kuvunja ndoa hii''-Alisema Jaji mkuu,Kimaru

Daisy alimshtaki Prezzo kwa kumnyanyasa kijinsia na kumuumiza mwilini..hata hivyo ndoa yao ilidumu miaka 4 kuanzia December 2008 walipofunga ndoa na kuishia November 2011 walipotalakiana
Jaji aliongeza pia unyama aliofanya Prezzo kwa mkewe sio jambo zuri kwa ndoa ya amani na maendeleo
Daisy aliiambia mahakama kuwa Prezzo alimnyanyasa kijinsia kwa kuwa na mahusiano na wanawake tofauti wakati wapo kwenye ndoa hasa Model wa zamani,Joy Wanjohi
Prezzo pia alimtukana Daisy kwa maneno machafu na kusababisha msongo wa mawazo..haikuishia hapo alimpiga mkewe na kushindwa kulipia majukumu ya kiuchumi

Mashtaka mengine Daisy aliyolalamika mbele ya mahakama ni mtalaka wake kunywa sana pombe na kutumia bangi muda mwingi wakiwepo pamoja
Akiwa anaelezea mkasa huo alisema Prezzo alialika rafiki zake kwenye nyumba waliojenga pamoja ambapo walikunywa pombe sana mbele yake na mtoto..mara nyingine alitoka na rafiki zakena kwenda kupombeka nje wakitumia 'madawa' kama bangi.
Akielezea kwa machungu,Daisy anasema kuwa muda mwingine ilibidi aombe msaada wa kiuchumi kwa wazazi wa Prezzo ili amuhudumie mtoto wao waliozaa pamoja
PREZZO NA MTOTO WAKE 

alipofungua kesi ya kuomba talaka,Daisy anasema Prezzo alikuwa anaishi nyumbani kwa mama yake baada ya malumbano ya maneno kwa muda mwingi..haikuchukua muda wa wiki moja na kusoma kwenye magazeti kuwa Prezzo anamahusiano ya mapenzi na Joy Wanjohi
Itakumbukwa kuwa January 2012,Prezzo alihojiwa na standard ambapo aliongelea shida ya ndoa yake,mapenzi na mahusiano na model wa zamani Joy Wanjohi ambapo aliambatana na mlimbwende huyo Joy Wanjohi
PREZZO NA JOY WANJOHI
Inasikitisha kuona Diva akishindana na Huddah kumtaka Prezzo kimapenzi wakati hawajui nyuma ya pazia anayofanya Prezzo na wangapi amefanya nao mapenzi..hadi leo hii Diva anaendelea kujianika mwili wake aonekane mrembo zaidi ya Huddah ili ateke mapenzi ya Prezzo
Previous
Next Post »