Mashindano ya kumtafuta mrembo Shinyanga yaani Miss Shinyanga Centre yamemalizika huku yakiingiwa dosari baada ya mshindi wa taji hilo SCOLASTIKA SITTA{19} kutoa malalamiko kuwa amedhalilishwa kwa kupigwa na kunywanganywa pesa kiasi cha shilingi laki 3 alizopewa ikiwa ni zawadi
mrembo huyo amesema tukio hilo limefanywa na muuandaaji wa mashindano ya miss Shinyanga ASELA MAGAKA baada ya mrembo huyo kukataa kuondoka kwenda Kahama usiku wa manane.
“Alitaka tuondoke baada ya kushuka jukwaani na twende Kahama kwaajiri ya kambi ya miss Shinynga usiku huo huo mimi nikakataa kwa sababu ilikuwa ni usiku sana na baada ya hapo akapanick akanipiga makofi na kuninyang'anya pesa zote shilingi laki 3”.Alisema mrembo huyo.
Mrembo huyo amesema kitendo hicho ni cha udhalilishaji na kimemkatisha tamaa ya kuendelea kushiriki mashindano kwa ngazi ya mkoa na amekwenda kutoa taarifa polisi na taratibu za kisheria zinaendelea.
Scolastica anatoa ushauri kwa waandaaji wa mashindano ya urembo kutowadhalilisha washiriki na kwamba warembo wanatakiwa kuwa imara na jasiri katika kudai haki zao na kupinga vitendo vya udhalilishaji kwani mashindano ya urembo yanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Nawashauri warembo wenzangu kusimama Imara na kutetea haki zao, tuungane kupinga udhalilishaji unaofanywa kwa mamiss” Alisema mrembo huyo.
Kwa upande wake muundaaji wa mashindano ya miss Shinyanga centre bi CHRISTINA STEVEN anasema kuwa tukio hilo hajalifurahia na limemharibia kwa sababu mrembo wake hataendelea mbele na mashindano ya mkoa.
ASELA MAGAKA ambaye ndie muundaaji wa mashindano ya miss Shinyanga, kwanza amekiri kumpiga miss huyo nakumnyang'anya pesa kiasi cha shilingi laki tatu na akasema kuwa alimwadhibu kama mototo wake baada yakuona kuwa wanaume wamemzingira na alikataa kuondoka kwenda Kahama kwa sababu alitaka kubaki na wanaume hao.
“Nimemwadhibu kama mtoto wangu kwa sababu mama yake mzazi alinikabidhi mimi huyo binti, na zile pesa amerudisha mwenyewe na ammeweka sahihi yake alisema yeye hatashiriki na atachukua mizigo yake.” Alisema ASELA.
EmoticonEmoticon