BAADA YA KUSIKIA MWILI WA MWANAE UMESHINDWA KUWASILI NCHINI, MAMA MANGWEA ANGUKA GHAFLA ALAZWA HOSPITA YA MKOA


            Bi Denisia Mangwea.mama mzazi wa msanii Albart Mangwea
      MAMA mzazi wa  marehemu Albart Keneth Mangwea Bi Denisia Mangwea[63] leo asubuhi ameanguka ghafla baada ya kupoeka taarifa kwamba mwili wa mtoto wake Albeth umeshindwa kuwasili nchini ukitokea Afrika ya kusini.Mtandao huu leo mchana ulipokea taarifa z a tukio hilo  ambapo  ambapo dada mkubwa wa Albeth Bi Magreth Mangwea alipoulizwa alithibitisha mama yake kuanguka ghafla baada ya kusikia mwili wa mpendwa mtoto wake umeshindwa kuwasili  nchini.
" Ni kweli leo asubuhi mama alipoamka tu kauli mwili wa mwanae umeshafika Dar es salaam alipoambia bado haijasika aliangua kwa presha na kwa sasa amelazwa hospita ya mkoa wa Morogoro akiendelea na matibabu mchna huu nimetoka huko amezinduka na anaendela vizuri kwa sasa na kwamba muda wowote anaweza kutolewa hospital"alisema Bi Magreth huku akiangua kilio.Mwandishi wa habari hizi alifika katika hospital hiyo na kukuta mama huyo mtaratibu akijianda kupewa ruhusa ya kurejea nyumbani Kwa taarifa zaidi endelea kutembea mtandao huu ambao kwa sasa umetega mitambo yake nje ya hospital hiyo ukisaka picha za mama huyo akiwa eneo hilo la hospital. 
Previous
Next Post »