WASANII WAHAIRISHA SHOO KWA SABABU YA KIFO CHA NGWAIR




Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini akiwemo Mwana Fa, Izzo  Business, pamoja na Kara Pina wamehairisha shoo zao ambazo zilikuwa zinatarajia kufanyika Mei 31 mwaka huu kwa sababu ya kifo cha msanii mwenzao Albert Mangwea kilichotokea jana nchini Afrika ya Kusini.

Mwana Fa ambaye alitarajia kufanya onyesho lake alilolipa jina la The Finest mwishoni mwa wiki hii amejikuta akiahirisha shoo hiyo kwa sababu ya msiba wa msanii mwenzao

Kwa upande wake Izzo Business alieleza  sababu ya kuahirisha shoo hiyo, alisema kuwa hawezi kuendelea na ratiba ya shoo hiyo wakati yupo katika wakati wa majonzi kwa kumpoteza msanii wao ambaye pia ni rafiki yao mpendwa .
Previous
Next Post »