WILAYA YA MBARALI - AJALI
YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA
KIFO.
MNAMO TAREHE 22.05.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA RUNWA BARABARA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI
T.840 ARY AINA YA M/FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA ALEX S/O BUTUSI MWANI, MIAKA
35,KYUSA, MKAZI WA UYOLE LILIMGONGA MPANDA BAISKELI ISIHAKA S/O GOLIAMA, MIAKA
90, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA RUNWA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI
AKIPATIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA .CHANZO KINACHUNGUZWA .
DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 22.05.2013 MAJIRA YA SAA 21:05HRS HUKO IYUNGA
DARAJANI BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI T.441 BYW/T496
BWD AINA YA SCANIA LILIENDESHWA NA DEREVA HERI S/O FAUSTINE,MIAKA 35,MNGONI
MKAZI WA MAMA JOHN MBEYA LILIGONGA PIKIPIKI T.815 BKQ AINA YA KING FAN
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA ABDALAH S/O EDWARD,MIAKA 41, MWALIMU WA SHULE YA
SEKONDARI IYUNGA MKAZI WA IYUNGA DARAJANI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO .
CHANZO NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA AMEKAMATWA GARI LIPO KITUONI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI
ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA
NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 22.05.2013 MAJIRA YA SAA 16:50HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MWIJI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA SEGULE S/O SHAGEMBE,MIAKA 2I,MSUKUMA,MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA
MWIJI AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI LENYE UKUBWA WA NUSU EKARI .MBINU ILIYOTUMIKA NI KULIMA BHANGI HIYO KWA KUCHANGANYA PAMOJA NA MAZAO MENGINE .
MTUHUMIWA NI MKULIMA NA MUUZAJI WA BHANGI TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI
- KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 22.05.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO KATIKA
ENEO LA KALOBE JIJINI MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA 1. EMANUEL S/O MSAKI, MIAKA 21, MCHAGA
NA 2. BROWN S/O SEME,MIAKA 22,MNDALI,WOTE
WAKAZI WA KALOBE WAKIWA NA BHANGI DEBE MBILI NA NUSU PAMOJA NA KETE 160 ZA
BHANGI SAWA NA UZITO WA KILO 5 NA GRAM
800 . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA BHANGI HIYO CHUMBANI. WATUHUMIWA NI WAUZAJI
NA WAVUTAJI WA BHANGI WAMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA
NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon