TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI PRESS RELEASE” TAREHE 15. 05. 2013


WILAYA YA MBEYA VIJIJINI - AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUGONGA PIKIPIKI  

  NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 14.05.213 MAJIRA SAA 11:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWANSEKWA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA BARABARA YA MBEYA/CHUNYA. GARI T. 405 BWA AINA YA ZHONGJI DUMPER   MALI YA KAMPUNI YA KICHINA YA UJENZI WA BARABARA IITWAYO CCCC LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA LILIGONGA PIKIPIKI T.605 ANP AINA YA TUK TUK ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA JUMANNE S/O NDELE,MIAKA 24,MSAFWA,MKAZI WA MWANSEKWA ILIYEKUWA AMESIMAMA PEMBENI YA BARABARA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU WALIOKUWA NDANI YA GARI HILO AMBAO NI  1. FILIMON S/O MGUMBE,MIAKA 30,MGOGO,MKULIMA MKAZI WA ITIGI 2. BARAKA S/O PAULO MWASOTA,MIAKA  24,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA MWANSEKWA NA 3. MWANAUME ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI UMRI KATI YA MIAKA 25-30 .  AIDHA KATIKA TUKIO HILO WATU WANGINE WANNE  WALIJERUHIWA  KATI YAO WAWILI WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA MAJERUHI WAWILI DON FUNG S/O CHENG,MIAKA 38  RAIA WA CHINA NA MWANAUME  MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA  JINA WALA MAKAZI YAKE KWA KUWA HAWEZI KUONGEA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.  MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI MWENDO KASI .DEREVA ALIKIMBIA NA KUTELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWANYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO DEREVA ALIYESABABISHA AJALI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA DHIDI YAKE ZICHUKULIWE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MARA MOJA.

 WILAYA YA RUNGWE – KUFANYA VURUGU NA KUHARIBU MALI

MNAMO TAREHE 14.05.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA WAZAZI LUPATA – WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. BWENI MOJA LA WANAFUNZI WA KIUME LILICHOMWA MOTO NA BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE HIYO NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI MBALIMBALI. CHANZO CHA TUKIO NI BAADA YA MWANAFUNZI WATATU WA KIUME KUSIMAMISHWA MASOMO KWA UTOVU WA NIDHAMU AMBAO NI 1.JOSEPH S/O ROBERT,MIAKA 18,MKURYA,MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE MKAZI WA KITUNDA DSM 2.MWITA S/O CHACHA,MIAKA 17,MKURYA,MWANAFUNZI KIDATO CHA TATU, MKAZI WA KITUNDA DSM NA 3. DANIEL S/O DAVID,MIAKA 18,KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA TATU MKAZI WA IPINDA KYELA  NA KUHAMASISHA WENZAO KUWAUNGA MKONO KUPINGA ADHABU HIYO  KWA KUFANYA VURUGU . BWENI LILILOCHOMWA MOTO WANAISHI WANAFUNZI 50 AMBAO HAWAKUWA TAYARI KUUNGA MKONO UVUNJIFU HUO WA AMANI. WATUHUMIWA KUMI NA TANO [15] WAKIWEMO JOSEPH S/O ROBERT NA MWITA S/O CHACHA  AMBAO WALIKUWA VINARA WA VURUGU HIZO WANAHOJIWA NA JESHI LA POLISI  . THAMANI HALISI YA UHARIBIFU ULIOTOKEA BADO KUJULIKANA. HAKUNA MADHARA YA KIBINADAMU YALIYOTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WANAFUNZI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WATATUE MATATIZO/KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA MEZA YA MAZUNGUMZO KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI KUEPUSHA MADHARA NA HASARA ZINAZOWEZA KUJITOKEZA AMBAZO MARA NYINGI WAHANGA WANAKUWA NI WANAFUNZI WANYEWE.

  WILAYA YA MBARALI – MTUHUMIWA MMOJA AKAMATWA NA MIFUKO 100 YA MBOLEA AINA  

YA CAN IKIWA KATIKA MIFUKO YA PREMIUM AGRO CHEMI LTD NDANI    

YAKE KUKUTWA MBOLEA IDHANIWAYO NI AINA YA MINJINGU.

·         MNAMO TAREHE 13.05.2013 MAJIRA YA SAA 13:00HRS ADJURIST S/O EDWARD NGEZI AFISA MAUZO KAMPUNI YA KUSAMBAZA MBOLEA IITWAYO PREMIUM AGRO CHEM LTD YENYE MAKAO YAKE MAKUU DSM ALITOA RIPOTI KITUO CHA POLISI MBARALI KUWA HUKO KATIKA MJI MDOGO WA CHIMALA WAKALA WAO WA KUSAMBAZA MBOLEA JOFREY S/O MBAGO ANASAMBAZA MBOLEA AMBAYO SIO HALISI KWA KUTUMIA MIFUKO YENYE NEMBO YA KAMPUNI YAO YA PREMIUM AGRO CHEM LTD.

 

·         KUFUATIA TAARIFA HIZO POLISI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANYA UPEKUZI KATIKA NYUMBA YA JOFREY S/O MBAGO PAMOJA NA STOO ANAYOHIFADHIA MBOLEA.

 

·         KATIKA UPEKUZI HUO POLISI WALIFANIKIWA KUKAMATA MIFUKO MIA MOJA [100] YA MBOLEA AINAYA CAN YENYE NEMBO YA PREMIUM AGRO CHEM LTD. HATA HIVYO UCHUNGUZI WA AWALI ULIOFANYWA NA EZBON S/O MICHAEL MBWANA, BWANA SHAMBA WA MJI MDOGO WA CHIMALA IMEBAINIKA KUWA NDANI YA MIFUKO HIYO KUNA MBOLEA INAYOSADIKIWA KUWA NI AINA YA MINJINGU, MBOLEA INAYOZALISHWA MKOANI MANYARA TOFAUTI NA PREMIUM AGRO CHEM LTD.

 

·         MTUHUMIWA ALIPOHOJIWA ALIKIRI KUWA MBOLEA HIYO AMEPELEKEWA NA WATU WAWILI AMBAO NI 1.SAMWEL S/O MHAVILE NA 2. ABSON S/O SANGA WOTE WAKAZI WA MAKAMBAKO MKOA WA NJOMBE NA KWAMBA MBOLEA HIYO INAUZWA KIASI CHA TSHS 50,000/= KWA KILA MFUKO WA KGM 50 NA MPAKA ANAKAMATWA ALIKUWA TAYARI AMEKWISHA UZA MIFUKO MINGI TANGU TAREHE 03.05.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS.

 

·         TARATIBU ZINAFANYWA ILI SAMPLE YA MBOLEA HIYO IPELEKWE KWA MKEMIA MKUU WA SERIKALI DSM ILI KUWEZA KUTHIBITISHA MIFUKO HIYO INA MBOLEA AINA GANI.

 

·         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA JAMII KUACHA TAMAA YA KUTAKA UTAJIRI WA HARAKA KWA KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA ZISIZO HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA KINAPOTEZA UAMINIFU KWA JAMII HASA WAKULIMA.

 

 

 

Signed By,

[ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »