MWANAFUNZI mmoja wa kike wa Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon ameshitakiwa Ijumaa kwa hali ya uvunjaji heshima na polisi wa kampasi baada ya Askofu Katoliki kulalamika kuhusu kutembea kwake hadharani akiwa uchi kuanzia kiunoni kwenda chini huku kavalia kama Papa.
Mwanafunzi mmoja wa kiume ambaye alikuwa uchi pia ameshitakiwa, lakini haikufahamika mara moja alichokuwa akifanya wakati wa gwaride la sanaa ya uch
oraji la majira ya bamvua ya Shule ya Pittsburgh mwezi uliopita.
Rais wa Chuo hicho, Jared Cohon alisema Ijumaa iliyopita kwamba mashitaka hayo madogo yalikuwa yamefunguliwa huko Allegheny County dhidi ya wanafunzi hao wawili na kwamba shule hiyo haitachukua hatua zozote zaidi za kinidhamu.
Alisema shule hiyo imebariki kujieleza kisanii lakini kujianika uchi hadharani ni kinyume cha sheria.
"Kuna ushindani wa thamani katika suala hapa: Carnegie Mellon inakusudia kuwa sehemu ambako mawazo yanaweza kuwasilishwa na kujadiliwa kwa uwazi, lakini pia ambapo watu wa historia zote, dini, na imani kujisikia wanakaribishwa na kupewa msaada," alisema Cohon.
Askofu David Zubik wa Dayosisi Katoliki ya Pittsburgh alilalamika baada ya gwaride hilo Aprili 18, ambapo mwanafunzi huyo wa kike - huku nywele zake za sehemu za siri zikiwa zimenyolewa kwa alama ya msalaba - alirusha kondomu kwa watazamaji. Cohon aliomba radhi wiki iliyopita kwa onesho hilo.
Chuo hicho hakikuwataja wanafunzi hao wawili. Rekodi za mahakama zinaonesha wanafunzi hao Katherine B. O'Connor, miaka 19, kutoka Pittsburgh, na Robb S. Godshaw, miaka 22, kutoka Wilmette, Illinois, walishitakiwa na polisi wa kampasi kwa tukio la uvunjaji heshima.
Hakuna mwanasheria aliyekuwa amejitokeza kumtetea yeyote.
Si O'Connor wala Godshaw aliyejibu ombi la kutoa maoni yoyote kuhusiana na suala hilo, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza Juni 10, mwaka huu.
Zubik alisema katika taarifa Ijumaa kwamba Chuo Kikuu hicho kinalichukulia 'tukio hili lisilotarajiwa' kwa uzito wa kipekee.
EmoticonEmoticon