ulinzi mkali wakati mbunge Msigwa na watuhumiwa wengine 70 wakifikishwa mahakamani leo
Wafuasi wa Chadema na wananchi wakiwa nje ya geti la mahakama leo
Watuhumiwa 70 wa vurugu za machinga na polisi mjini Iringa akiwemo mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa hivi sasa wanafanyiwa utaratibu wa dhamana baada ya mahakama kukubali kupewa dhamana baada ya kusomewa mashitaka matatu huku mbunge akisomewa shitaka la kushawishi watuhumiwa hao kufanya vurugu .
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka dhidi yao na kwa sasa utaratibu wa dhamana unafanyika mbele ya mahakama hiyo ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya .
Hata hivyo wamekana mashitaka yote yaliyotolewa ambayo shitaka la kwanza la mbunge ni kushawishi kufanya vurugu ,huku wengine wote kosa la kwanza kufanya mkutano bila kibali , kuharibu mali kinyume na sheria ni kufanya vurugu .
Hadi sasa baadhi ya watuhumiwa wana wadhamini na dhamana yao ni kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Tsh milioni 1 na kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.
Habari kamili inakujia hivi punde ila hadi sasa mdhamini wa mbunge Msigwa na baadhi ya watuhumiwa waliowengi wametimiza masharti ya dhamana
EmoticonEmoticon