KATI YA HAWA MMOJA ATATANGAZWA KWENDA BBA.

 

Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Jacqueline Patrick ‘Jack Patrick’ (pichani) , Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’  mmoja wapo ataungana na mwanaume kuiwakilisha Bongo kwenye Shindano la Big Brother Africa 2013 linalokwenda na kikolombwezo cha The Chase. 

 

Jack Pentezel

Kwa mujibu wa chanzo chetu (tunaficha jina lake), mastaa hao wa kike, mmoja ndiye ataibuka mshiriki kwa mwaka huu ambapo atakaa ndani ya mjengo kuanzia Mei 26, 2013 ambapo shindano litaanza rasmi. 

 

Jack Patrick

“Mimi nawamegea tu kwamba kati ya Wema, Baby Madaha, Jack wa Chuz na Jack Patrick  mmoja wao anakwenda Big Brother mwaka huu.

 

Wema sepetu

“Halafu ninachojua mimi, mshiriki ameshatumiwa taarifa kutoka Multi Choice, ila tatizo wale jamaa wanataka mtu msiri sana, mshiriki hatakiwi kumwambia mtu mpaka siku atakapoondoka,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Jumamosi lilipiga kiguu hadi Ofisi za Multi Choice jijini Dar na kuulizia Mbongo anayekwenda, likakumbana na majibu haya:


 

Baby Madaha

 

“Sisi pia hatujui. Unajua ilivyo ni kwamba huwa tunatuma majina, sifa na anuani za watu kama watano kule Sauzi, halafu wao wanaangalia vigezo vyao, anayeshinda anataarifiwa kutoka kulekule bila sisi kujua,” alisema mtumishi mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Risasi Jumamosi juzi Alhamisi liliongea na Jack wa Chuz ambaye alisema aliwahi kuombwa kushiriki shindano hilo kwa sababu ya ushombe wake lakini hakuweka wazi kama alijaza fomu za maombi au la!
Aidha, Baby Madaha alipoulizwa alikiri kujaza fomu za kukusudia kushiriki siku za nyuma akiwa sambamba na Wema lakini akasema hajui nani kashinda ingawa lazima mshiriki ameshapatikana kati yao.
“Nasikia mshiriki anatakiwa kujijua wiki tatu au mbili kabla. Kwa hiyo atakuwa tayari anajijua, inakuwa siri ya mtu, hakuna anayeweza kujitaja kwa watu,” alisema Baby Madaha.
Simu ya Jack Patrick haikuwa hewani siku hiyo huku watu wake wa karibu wakisema yupo nje ya Bongo kibiashara zaidi. Simu ya Wema muda mwingi iliita bila kupokelewa hadi mpigaji akachoka.
Kwa upande wa wanaume, wanaotajwa kushiriki shindano hilo mwaka huu ni staa wa sinema za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, nyota wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ na aliyewahi kuwa Mtangazaji wa Clouds TV, Rommy Jones ambaye ni ndugu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. 

 

Previous
Next Post »