NEWCASTLE YAAGA MASHINDANO, TOTTENHAM NAYO YANG’OLEWA KWA MATUTA

comment
MKWAJU wa Papiss Cisse uliozaa bao katika kipindi cha pili haukutosha kuiokoa Newcastle na hivyo kujikuta inatupwa nje ya michuano ya Europa League na Benfica ya Ureno huku Tottenham nayo ikiaga mashindano kwa matuta.
Mohamed Salah
 
Bao hilo la dakika 71 la nyota huyo wa Senegal lilidumu hadi dakika ya 90 pale Eduardo Salvio alipoizawazishia Benfica na mpira kumalizika kwa sare ya 1-1 lakini Benfica wakasonga mbele kwa jumla ya magoli 4-2 kufuatia ushindi wao wa 3-1 kwenye mchezo wa awali.
Sare ya 2-2 kati ya Tottenham na Basel ilipelekea mchezo huo kwenda dakika 30 za nyongeza na hatimaye hatua ya matuta. Katika mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya 2-2 na hivyo kufanya matokeo ya jumla yasomeke 4-4.
Clint Dempsey aliyekuwa nyota wa mchezo, aliifungia Tottenham goli la kwanza dakika ya 23, Basel wakachomoa dakika ya 27 kupitia kwa Mohamed Salah na baadae kuongeza bao la pili lililofungwa na Alexander Dragovic katika dakika ya 49.
Clint Dempsey akafufua tena matumaini ya Tottenham baada ya kuisawazishia katika dakika ya 82, kabla timu yake haijapata pigo la kumpoteza beki wake tegemeo Jan Vertonghen kwa kadi nyekundu.
Clint Dempsey
Kutolewa kwa Jan Vertonghen kwenye dakika ya 90 kukawafanya Tottenham wacheze wakiwa pungufu kwa dakika zote 30 za nyongeza hali iliyowaweka kwenye wakati mgumu hadi mwisho wa mchezo.
Katika hatua ya matuta Basel ikapiga penati nne na zote zikaenda wavuni huku Tottenham ikipoteza penalti mbili kati ya tatu ilizopiga. Tom Huddlestone na Emmanuel Adebayor ndio waliokosa penalti.
Kwa ushindi huo, hii inakuwa ni nusu fainali ya kwanza katika historia ya  Basel kwa michuano yote ya Ulaya.
Previous
Next Post »