RIHANA ASEMA YEYE NI MBUMBUMBU WA MAPENZI



“MIMI nipo katika kundi la watu ambao hawaelewi mapenzi.” Hiyo ni kauli ya staa wa muziki wa Pop wa Marekani, Rihanna akiwaambia mashabiki wake.
Rihanna alitoa kauli hiyo akiwa kwenye steji huko Los Angeles usiku wa Jumatatu iliyopita, akithibitisha uvumi kwamba ameachana tena na mpenzi wake Chris Brown.
 
Akihutubia umati wa watu katika shoo yake iliyopigwa ndani ya Staples Center, aliuliza: "Ni wangapi kati yenu wapo kwenye mapenzi? Wangapi kati yenu mnachukia mapenzi?
"Wangapi kati yenu hawaelewi  mapenzi? Mimi niko katika kundi hilo. "
Rihanna alitoa nafasi ya pili kwa mwimbaji Brown baada ya kumpa kichapo kikali mwaka 2009.
Brown alihukumiwa ‘kifungo cha nje’ miaka mitano, huku akitakiwa kufanya kazi za jamii kwa saa 1,400 kutokana na kitendo chake hicho.
Hata hivyo, nyota hao walizika tofauti zao na kutangaza kurudiana mwezi Februari mwaka huu.
Previous
Next Post »