MSANII WA FILAMU SINGLE MTAMBALIKE RICH RICH AFANYA BALAA KATIKA SAFARI YA TANGA..IREN UWOYA,CHOPA NA GABO ZIGAMBA,CHUCHU HANCY NDANI

Wakiwa katika pozi ndani ya location yenyewe huko Tanga
 
Moja ya scene iliyopo katika filamu hiyo ya safari iliyochezewa Tanga maeneo ya Amboni
 Msani mkongwe ndani ya gemu la filamu ambaye makali yake hayashuki hadi leo single mtambalike au Richi Richi amendelea kuonyesha kuwa yeye bado atabakia kuwa mwalimu wao katika gemu hili la filamu nchini tanzania kwa kutowa kazi zenye ubora na zinamfanya awe juu kila kukicha.Msanii huyu mkali ambaye alishaitwa na wachezaji maarufu wa tamthilia nchini afrika ya kusini kwa wakati ule egoli na kujifunza mengi yanayohusu filamu amesema kwa sasa yupo mbioni kuachia filamu yake mpya aliyomshirikisha irene uwoya,juma chikoka gabo zigamba,chuchu hansi Libaty msusaya na wengine kibao ambao wamekamua vya kutosha ndani ya filamu hiyo


Akizungumza na thesuperstarstz maeneo ya nyumbani kwake ilala singo amesema kuwa kwasasa haitaji maneno badala yake anataka mashabiki ndio waseme watakachokiona ndani ya filamu hiyo mpya rich ameendelea kuweka wazi kuwa amejipanga kufanya filamu zenye mabadiliko kwani yeye sio wakucheza filamu za aina moja na ndio maana katika movie watu wamtegemee rich mwingine kabisa katika makamuzi

Rich ameiambia thesuperstzrstz kuwa anawashukuru sana watu wa amboni tanga iliposhutiwa filamu hiyo na kusema ni wa karimu sana na kwa hakika walimpa ushirikiano wa kutosha,Filamu hiyo inayokwenda kwa jina la SAFARI Huku story akiwa kasimama Mbarikiwa na Rich mwenyewe na kwa upande wa Director akiwa kasimama Rich Rich.

Picha  ya pozi katika filamu hiyo
Filamu ya safari inatarajiwa kutoka muda wowote ule na kwasasa zimebaki hatua chache sana alisema edtor wa rich anayejukana kwa jina la koba ambaye ndiye anayepika mzigo huo hapo hapo ofisini kwa rich maeneo ya ilala mtaa wa pangani.

Previous
Next Post »