MANGULA KUFUNGA PINGU YA MAISHA , WAZIRI PINDA MGENI RASMI


 
BW. Mangula 

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania bara Philip Mangula, anatarajia kufunga ndoa siku ya jumamosi wiki hii kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) mjini Njombe.

Mwandishi  wa mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Njombe Shaban Lupimo amefanya mahojiano na  msemaji wa familia ya mzee Mangula, mhadhili wa chuo kikuu huria Tanzania tawi la Njombe Dk. Lechion Kilimike ,  hili leo  kuwa ndoa ya Mangula itasimamiwa na Askofu Mstaafu wa Solomon Swalo wa KKKT diyosisi ya kusini.

Alisema mgeni wa heshima katika zoezi hilo anatarajiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye atashududia zoezi hilo na mara baada ya ndoa kufungwa ataelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya kikao cha
bunge la bajeti.


 

                             Bw Pinda
Alisema Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kufika hapa mkoani kesho majira ya saa saba mchana tayari kwa ajili ya kushuhudia  ndoa hiyo kesho
kutwa.


“Ndoa ya mzee Mangula itafungwa majira ya saa tatu asubuhi, itafungishwa na Askofu Mstaafu Solomon Swalo wa KKKT dayosisi ya kusini, lakini mgeni wa heshima katika dhifa hiyo atakuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda,” alisema Dk. Kilimike.


Dk. Kimile alisema Mzee Mangula anamuoa mkuu wa shule ya sekondari ya Philip Mangula iliyopo weilayani Wanging’ombe mkoani hapa Yolanda
Kaberege.


Hatua hiyo ya mzee Mangula kuoa inakuja kufuatia aliyekuwa mke wake wa ndoa kutangulia mbele za haki mwaka 2004.
Previous
Next Post »