MREMBO ALIYEKUTWA AKITUPA TAKA OVYO MANISPAA YA IRINGA APEWA ADHABU YA KUFANYA USAFI WA MJI

 

 Bwana  Afya  Manispaa ya  Iringa Aron Mafumiko akimtaka mrembo  huyo  kuonyesha takataka alivyokutwa akitupa ovyo leo
 Hapa Mrembo  huyo Eliza  Luvinga  akiangua  kilio  kuomba asilipishwe faini ya Tsh 50,000 kama  sheria  ya Manispaa ya Iringa inavyoagiza kwa wanatupa taka taka  ovyo
 Hapa  akipelekwa kufanya usafi badala ya  kulipa  faini
 
 Kazi ya kuzoa  taka taka  ikiendelea kama sehemu ya adhabu mbadala baada ya  kuomba asitozwe Tsh 50,000
 
 Hapa  akielekea  kumwaga  taka katika chombo maalum cha kuhifadhi taka kata eneo la bustani ya manispaa ya Iringa
 
 Hapa akimwaga  takataka  chini  ili  kuzihifadhi katika  chombo chake
kazi ya  kuhifadhi taka  eneo husika  ikifanyika na mrembo  huyo mkazi  wa Ndiuka katika Manispaa ya Iringa .
.........................................................
Wananchi  wa Manispaa ya  Iringa  wameanza  kutoa ushirikiano kwa  uongozi  wa Afya  wa manispaa ya  Iringa  katika utekelezaji  wa sheria  ndogo ya usafi  inayowataka  kuwakamata  watu  wanaotupa taka taka  ovyo na  kuwafikisha katika ofisi wa Manispaa ili walipe faini ya Tsh .50,000 na yule aliyekamata  kunufaika na motisha ya  Tsh 20,000 kati ya  fedha hizo za faini.
Mtandao  wa  www.francisgodwin.blogspot.com umeshuhudia  mrembo mmoja aliyefahamika kwa jina la Eliza Luvinga  akikamatwa na wananchi na kufikishwa  ofisi ya  Afya  Manispaa ya Iringa ili kutozwa  faini  hiyo .
 
Hata  hivyo  mrembo  huyo ambae ni mkazi  wa Ndiuka katika Manispaa ya Iringa alilazimika  kuangua kilio  kuomba  kupunguziwa adhabu  kutoka  faini ya  Tsh 50,000 na kufanya kazi ya  kusafisha mji  wa Iringa .
 
Kutokana na huruma ya  wananchi  waliomkamata  mrembo  huyo  waliomba  oungozi  wa afya Manispaa ya Iringa  kumpa adhabu  hiyo ya kusafisha mji kutokana na kuangua  kilio  kuwa hana uwezo  wa kulipa  pesa hizo kutokana na kutokuwa na kazi ya kufanya.
 
Akizungumza na mtandao   Bwana  Manispaa ya Iringa Aron Mafumiko  mbali ya  kuwapongeza  wananchi kwa kuanza kuchukia uchafu  bado alisema  sheria ipo kwa  watu  wanaochafua mji pale wanapokamatwa  kutozwa  kiasi cha shilingi 50,000 na kati ya  fedha  hizo mkamataji hulipwa Tsh 20,000 kwa kazi  aliyoifanya na kuwataka  wananchi  kusaidiana na Manispaa kuwakamata  wale  wote  wanaotupa taka  ovyo
Previous
Next Post »