DU JANA TIMU ZA YANGA NA SIMBA ZA BONGO MOVIE MBONA ZILIPATA WASHANGILIAJI HEBU JIONEE MWENYEWE

   
Kama uli-miss kufika kwenye mechi hii usikonde wala usiwaze, hii hapa full coverage ya vitu kibao ambavyo hata watu wengine waliokuwa pale hawajaviona. Sikukuu ya muungano imesherekewa kwa njia tofauti na watu mbalimbali, Bongomovie nao waliandaa mechi kali maeneo ya Leaders Club ambapo timu mbili za BongomovieTeamYanga ikamenyana na BongomovieTeamSimba. Wananchi kibao kama kawaida walitia maguu kuja kucheki game na ku-mingle na mastaa wa bongomovie.
RAY AKIZUNGUMZIA  MECHI HII

TIMU ZINAINGIA UWANJANI
Yanga walianza na ngoma na vuvuzela za kutosha…Timu ilikuja na basi la Yanga full njano mwanzo mwisho.Shughuli nzima ya uishangiliaji ikiongozwa na Mboto ,Irene uwoya,Shilole,Rado,Bi Mwenda na wengine. Baada ya dakika chache akaja TeamYanga mwingine, huyu ni maarufu kwa kukata mauno sana mzee mwenyewe Richie.Akaanza kushangilia hata kabla hajashuka kwenye gari, alivyotoka tu akapanda juu ya gali na kilichofuata unakiona hapoa chini
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Kwa ujumla Yanga Bongomovie ni Mama Loraa,Shilole,Rado,Ray,Wolper,Mboto,Irene Uwoya,Barafu,Jini Kabula,Richie,Bi Mwenda,Claudi 112,OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA
SIMBA WANAINGIA
Mbwebwe zinaendelea na JB Bonge la bwana ndiyo manager wa Simba ya Bongomovie basi mambo yakawa ki-don zaidi. Basi moja lilibeba mashabiki wa Simba bongomovie na wachezaji wakaingia uwanjani na Limousine nyeusi kama wanaenda kwenye wedding, akashuka JB bongo la bwana watu wakajua JB ndiyo kaja na gari lote lile. Mara hizooo jezi nyekundu zinatoka wakiongozwa na capten wao William Mtitu mmiliki wa kampuni ya 5 Effets.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA
REFA KACHELEWA
Timu zimechelewa kufika hasa Simba na refa naye ndiyo kachelewa zaidi. Mechi iliisha wakati giza limeshaingia yote kwasababu ya vitu kuchelewa kuanza. Sasa ikabidi mahasimu wawili Simba na Yanga wakutane ili kufanya mawasiliano refa yuko wapi, bahati nzuri hakuwa mbali na kipute kikaanza baada ya timu zote mbili kusalimiiana.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA
SIMBA NA MBWEMBWE NYINGI
Kama unajua style ya kushangilia ya timu yenyewe ya Simba ya “Kidedea”..basi hapo ilikuwa inapigwa sana na kwasababu ilikuwa rahisi kuitikia hata wananchi nao hawakuwa nyuma kuitikia. Wakina dada wa BongomovieTeamSimba wakiongozwa na Shamsa Ford,Chuchu Hans,Aunty Ezekiel,Odama waliongoza shangwe za kidedea hadi waponyamazishwa na goli la Ray Kigosi.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA
GOLI LA KWANZA
Jezi nambati tisa mgongoni director Ray Kigosi na captain wa BongomovieTeamYanga anatupia wavuni goli la kwanza na Bonge la bwana JB anatulizwa kimya na timu yake yote. Lakini sipati picha kama TeamYanga wangefungwa hili goli ingekuwaje, goli moja wakina dada wa TeamYanga wanawatambia wenzao wa TeamSimba hadi sehemu yao ya benchi. Fikiria kasi ya ushangiliaji ikiongozwa na Shilole,Jini Kabula,Irine Uwoya,Bi Mwenda….full shwangwe hapo.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
HALF TIME(MAPUMZIKO)
Goli ni moja bila, Ray akiwa kaibeba TeamYanga. Wakati wa mapunziko TeamYanga wanaonekana kutokulizika na bao moja. Mmoja kati ya wadau wa benchi la ufundi mzazi Barafu anawachana kwamba kiungo bado hamjakaa vizuri kwasababu mipira inafika mara chache sana mbele.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERA OLYMPUS DIGITAL CAMERAAnakuja kocha na yeye anaongezea yake eti hawa wetu tu, kuna bao nyingi hapa tukiendelea kuwakazia hawa jamaa.
Upande wa Simba, Chiki akiwa na JB na washkaji wengine wa TeamSimba wanawapa moyo wachezaji..ohh hawa wetu tu, badi hatujawachezea game ya kinyama kama mnyama mwenyewe Simba.Kila mtu anamjua yule kipa, hamna kitu pale. Sogeeni karibu tu na goli mpango mzima tu walaza hawa jamaa.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Ali Choki mzee wa farasi enzi hizo na siku hizi ni mzee wa Extra Bongo na yeye anafunguka yake kui-support TeamSimba…Pyeeee…kipindi cha pili kinatakiwa kuanza.OLYMPUS DIGITAL CAMERA
KIPINDI CHA PILI
Kipindi cha pili TeamSimba wakaanza kwa kasi sana na jamaa mmoja anajulikana kwa jina la KIDUKU akatupia kimyani goli la kusawazisha. Kidede pale kati ikaanza kwa kasi sana.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
Simba kapakatwa: Goli la pili likitupiwa wavuni na Haji likaipa ungozi wa mechi TeamYanga na captain Ray Kigosi akatoa sub kwa mchezaji mwingine.OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
LIBOLO LIBOLO LIBOLO LIBOLO
Kama unakumbuka timu ya Simba ilifungwa na Libolo, baada ya hapo ikawa utani mkubwa kwa wapenzi wa Simba. Basi hata kwenye mechi hii, TeamYanga ilikuwa inajibu mapigo ya wimbo wa Kidedea kwa wimbo wa Libolo,Libolo,Libolo huku ngoma ikinogeshwa na mikono yote juu.
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
CHOPA ASALITI TIMU NA YAMKUTA MABAYA
Wakati anaingia uwanjani alikuwa anaonekana ku-support teamsimba.Goli la kwanza lilivyoingia, akavumilia..wakarudisha akaendelea kuruka na TeamSimba wenzake. Baada ya kupigwa goli la tatu na kuona mambo yashaenda kombo kwamba mzigo hautarudi tena. Akaanza kusaliti team yake ya Simba na kuanza kujipendekeza Yanga..unajua walichomfanya madada wa yanga. Cheki hapo
Previous
Next Post »