BAADA ya zile dawa za
Kichina za kuongeza makalio, ‘hips’ na matiti zilizotikisa Bongo na kubainika
kubeba madhara makubwa kama vile ‘kalio’ moja kuwa kubwa kuliko lingine, kujazia
zaidi chini kuliko juu na mwili kufa ganzi, zilikosa soko, lakini sasa zimeibuka
nyingine za kienyeji
Uchunguzi uliofanywa unaonesha kwa wataalam mbalimbali wa tiba za asili TANZANIA ,
ulibaini kuwa dawa hizo zimejaa tele kwa waganga wa kienyeji.
Ilifahamika pia kuwa hivi sasa dawa hizo
zinachangamkiwa na wanawake ile mbaya wakiamini kwamba hazina madhara kama zile
za Kichina.
NI MCHANGANYIKO WA MITI
60
Mmoja wa wataalam hao aliyezungumza na
audifacejackson blogalisema kuwa, dawa hiyo ni mjumuisho au mchanganyiko wa miti
zaidi ya 60 inayopatikana kwenye misitu mikubwa hasa mikoani.
UNACHAGUA KALIO
UNALOTAKA
Mtaalam huyo alikwenda
mbele zaidi na kuweka kweupe kuwa dawa hiyo ni kiboko ya Mchina kwani dozi na
bei yake hutegemea aina ya kalio analolitaka mteja husika.
“Ukitaka dogo, la kati au kubwa, kila moja
lina dozi na bei yake hivyo inategemea mteja amechagua la aina
gani,” alisema mtaalam huyo. WATAALAM WA TIBA ASILIA
WANASEMAJE?
waandishi wa
audifacejackson blog waliendelea kufanya mahojiano na wataalam mbalimbali wa
tiba za asili ambapo walikuwa na haya ya kusema:
MJUKUU WA BABU
Mganga maarufu kwa jina la Mjukuu wa Babu
anayepatikana Mwananyamala jijini Dar es Salaam alifunguka:
“Nakwambia hii dawa ni kiboko ya zile za
Kichina. Ni dawa nzuri na kusema kweli watumiaji ni wengi. Ni mchanganyiko wa
miti zaidi ya sitini ambao huwa unatoa aina moja ya dawa.
EmoticonEmoticon