WEMA AMSAINISHA KAJALA ENDLESS FAME....SOMA ZAIDI HAAPA
Habari mpya kitaa kwasasa ni kwamba Queen wa Bongomovie Wema Sepetu amemsign Kajala kufanya kazi chini ya uangalizi wa kampuni yake ya Endless Fame.
Wema amesema kwamba hadi kufikia sasa Kajala anafanyia kazi Script ya filamu yake mpya inayoitwa ‘Princess Sasha’ ambayo tayari imeshaanza kumulikwa na huenda kazi yote ikamalizika siku ya jumalipili.
Aidha kufuatia uvumi kuwa Wema anamtumia Shostisto wake Kajala kurudisha kiasi cha pesa alichogharamia katika dhamana yake Star huyo amekanusha vikali na kusema kwamba hakuna ukweli dhidi ya tetesi hizo.
Wema amesema amemsign kajala kama actress mkali ambae anaamini kiwango chake kizuri katika kazi za uigizaji na kuongeza kuwa hata sasa watakapofanya kazi ya kufyatua filamu atamlipa kama ambavyo angefanya kwa msanii mwingine.
Star huyo amesema kuwa filamu ya ‘Princess Sasha’ itakuwa inahusu story ya mtoto wa mfalme nafasi ambayo itachezwa na kajala akiwa kama main character na kutakuwa na mambo mengi yakuvutia ambayo yatatokezea baadae kwenye hadithi ya filamu hiyo.
EmoticonEmoticon