FERNANDO TORRES ameendelea kuwa katika kiwango bora wakati Chelsea ilipofanikiwa kupenya hatua ya nusu fainali ya Europa League (Ulaya ndogo) licha ya kucheza mchezo wa kujihami na kulala 3-2 dhidi ya Rubin Kazan.
Kufuatia ushindi wake wa nyumbani (Stamford Bridge) wa 3-1 katika mchezo wa awali, Chelsea inasonga mbele kwa jumla ya magoli 5-4.
Torres aliiandikia Chelsea bao la kuongoza dakika ya tano kufuatia pasi murua ya kiungo Frank Lampard lakini Ivan Marcano akasawazisha muda mfupi baada ya kuanza kipindi cha pili.
Victor Moses akaipeleka tena mbele Chelsea kabla ya Rubin Kazan kucharuka na kupiga mabao mawili kupitia kwa Gokdeniz Karadeniz na Natcho.

EmoticonEmoticon