SUALA LA TALAKA BADO LAMUSUMBUA TOM CRUISE



TOM Cruise akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuachana na mwigizaji mwenzake, Katie Holmes, amekiri kuwa hakutarajia kama wangepeana talaka.
Supastaa huyo aliachana na Katie mwenye umri wa miaka 34 mwezi Juni mwaka jana, siku tano kabla kusherehekea ‘birthday’ yake, akitimiza miaka 50 ya kuzaliwa.
 
Akizungumza na Kituo cha Televisheni ya Ujerumani, Cruise alisema: "Maisha ni changamoto. Una miaka 50 na unafikiri una kila kitu katika mpangilio wake, na ghafla inakuumiza – hivyo ndivyo maisha yalivyo.”
Wawili hao walio miongoni mwa watu maarufu duniani, walidumu kwenye ndoa miaka sita na wamejaliwa kupata mtoto mmoja, binti aitwaye Suri mwenye umri wa miaka sita sasa.
Wakati Suri akibaki na mama yake mjini New York, Cruise na Katie wanashirikiana kumlea.
Cruise aliongeza: "Maisha ni kama komedi ya kutisha, unahitaji hali ya furaha."
Cruise alizungumza hayo wakati akitangaza ujio wa filamu yake mpya, Oblivion, ambayo pia imewashirikisha mastaa Olga Kurylenko na Morgan Freeman.
Previous
Next Post »