Leo asubuhi baada
ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo
ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa
nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa
juzi na Naibu Spika. Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu
vjambo hilo uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye
kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale
itakapotokea tukio kama hilo.
Kwa uamuzi huo
Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana),
Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo
Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa
kumtoa nje Mh. Lissu, Mh. Sugu na wengineo, na kupewa adhabu ya kutoshiriki
vikao vitano vya Bunge, Kutokana na Mh. Tindu Lisu Kuomba Muongozo/Taarifa mara
kwa mara, Hivyo Kuingilia wengine katika kutoa hoja zao, na baadae kitendo cha
wabunge hao kukaidi amri Halali ya Naibu Spika ya kutoka nje ya Bunge pamoja na
kuwagomea Askari wabunge, kitendo ambacho kidogo kizue masumbwi live,
Umebarikiwa na Mheshimiwa Spika kwa kufuata kanuni za Bunge, Hivyo Basi,
Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu
iliotolewa.
Taswira ya vurugu
zilizotokea bungeni dodoma jana ambapo Mbunge wa mbeya Mh mbilinyi akiskiwa
pamoja na wenje, lema na wengineo wakionekana kwa pamoja wakiwazuaia askari ili
wasimtoe nje mh Tundu lissu aliyeamriwa na naibu spika atolewe nje ya ukumbi wa
bunge
hapa waziri wa nchi na uratibu wa bunge Mh William Lukuvi akiwaeleza jambo wabunge wa chadema mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa baada ya kutokea vurugu bungeni
EmoticonEmoticon