Wagonjwa kuanza kulipia malipo benki- Muhimbili sasa nauliza ndio mbinu mbadala kukabiliana na hao wabadhilifu ama kusumbua wagonjwa na je malipo yatafanyika baada ya matibabu ama haya ni masali yangu binafsi

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, imetangaza kuboresha huduma zake ambapo wagonjwa wataweza , kulipia gharama za huduma kupitia benki kuanzia Machi 11 mwaka huu.



Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Marina Njelekela, wakati alipokuwa akizungumza na vyombo va habari kubainishga mikakati hiyo

Amesema lengo la mkakati huo ni kudhibiti ufisadi na na ubadhirifu unaoendela kutoka hospitalini hapo unaofanywa na baadhi ya watendaji

Amesema uchunguzi umebaini hatua ya kutumia benki katika kukusanya malipo ya gharama za huduma mbalimbali, itasaidia kuokoa zaidi ya asilimia 20 ya fedha ambazo zimekuwa zinapotea

Pia mkakati huo utasaidia kupunguza mrundikano wa wagonjwa,uliopo hospitalini hapo ambao wengi hutoka mikoani

Amesema hospitali hiyo imeingia makubaliano na Benki ya NMB, ili kutekeleza mkakati wa kukusanya mapato yake

 
Previous
Next Post »