HIKI NDICHO ALICHOKISEMA HASHIMU KAMBI KUHUSU FILAMU ZA KITANZANIA NCHINI GHANA

 


Hashim Kambi akiwa na wasanii wakubwa wa Ghana
 
Swahiliworldplanet ilipata chance ya kuchonga na actor wa Tanzania Ramsey Hashim(Hashim Kambi) ambaye anafanya filamu na mastaa wakubwa wa Ghana Van Vicker na John Dumelo kuhusu tofauti iliyopo kati ya filamu za Swahiliwood na Ghana ,kama filamu na waigizaji wa Tanzania wanajulikana Ghana, pia nini cha kujifunza kutoka kwa wenzetu hao ambao wapo mbele yetu. na amejifunza nini huko Ghana? Hashimu Kambi alijibu hivi....

" Labda nianze kwa kusema kuwa filamu zetu za kitanzania hazijulikani kabisa nchini Ghana na kwa misingi hiyo basi ni kwamba hakuna msanii hata mmoja wa Tanzania anayejulikana nchini Ghana, hivyo tuna kazi kubwa kwa hilo. Nimejifunza mengi kwa mimi kuwa Ghana na kufanya kazi na wasanii wakubwa wa nchini Ghana kubwa likiwa ni kuhakikisha wanatoa filamu yenye ubora, hivyo wanahakikisha kuwa kabla ya kuanza shooting wanahakikisha kuwa wanafanya setting ya muda mrefu kuhakikisha kuwa itapatikana picha nzuri na sauti pia nzuri, sio hapa kwetu tukiseti kwa dakika 10 tunaanza shooting na pia Director anakuwa na wajibu mkubwa kwa kila kitu wakati wa shooting lakini pia hawana haraka kutaka kumaliza shooting haraka na ndio maana kwa siku wanaweza kushoot scene 5 tu wakati huku tunataka tushoot scene 13. Vifaa wanavyotumia tangu Camera,taa na hata vifaa vya sauti viko katika hali nzuri kabisa na hakuna waya za kuungaunga.

Pia kuna tatizo kwenye lugha na ingawa tunaweka subtitle ya kizungu pale chini kuna baadhi ya filamu hiyo subtitle inakuwa haiendani kabisa na story ya movie"

Watengeneza filamu za kitanzania nafikiri tumeona na kusoma alichokisema Hashimu Kambi hivyo tujifunze kutoka kwa wenzetu ili tupige hatua zaidi.
Previous
Next Post »