STEVE NYERERE KUTENGENEZA FILAMU YA SHILINGI MILIONI 60

STEVE NYERERE KUTENGENEZA FILAMU YA SHILINGI MILIONI 60

MSANII wa filamu za kibongo na mmoja wa wachekeshaji vinara, Steve Nyerere amesema muda wowote kuanzia sasa ataanza kazi ya kurekodi filamu yake mpya itakayogharimu zaidi ya milioni 60 za Kitanzania.
Steve Nyerere amesema filamu yake itavunja rekodi ya vitu vitatu: gharama kubwa, idadi kubwa ya washiriki na la mwisho ni muda mrefu wa kutengeneza filamu.
Akiongea na Saluti5, Steve amesema mbali na kutumia zaidi ya milioni 60 lakini pia filamu yake itawashirikisha zaidi ya washiriki 50 huku ikuchukua muda usiopungua miezi miwili katika uchukuaji wa picha kabla ya kuingia kwenye hatua ya uhariri.
Amesema yote hayo hayajawahi kufanyika katika sinema za kibongo.
Steve ameitaja filamu hiyo kwa jina la “Goodbye Mr President” ambayo ataigiza kama Rais Kikwete.
“Hii si filamu ya kitoto, itakuwa na vitu vingi vitakavyoonyesha uhalisia wa kile tunachoigiza” alitamba Steve Nyerere.
Previous
Next Post »