JAY Z, BEYONCE WAFANYIWA VIBAYA



Jay Z pamoja na Baby Mama wake Beyonce Knowles, wameingia katika maswahiba mengine hasa baada ya watu wasiojulikana kuiba taarifa zao binafsi ikiwepo anuani zao namba za account na taarifa zao nyingine za benki pia.
Wahalifu hawa ambao ni wataalam wa technolojia maarufu kama - Hackers, wameenda mbali zaidi na kuwafanyia uhuni huu pia Makamu wa Rais wa Marekani, Bwana Joe Biden pamoja na aliyekuwa waziri wa mambo ya nnje wa nchi hiyo Bi. Hillary Clinton.

Joe Biden
Hillary Clinton

Mastaa wengine ambao wameathirika kwa issue hii ni pamoja na Kim Kardashian, Ashton Kutcher, Mel Gibson, Paris Hilton na wengineo.

Kim Kardashian
Ashton Kutcher
Mel Gibson
Paris Hilton

Wahuni hawa hawa ndio waliohusika katika kuvujisha orodha ya ngoma ambazo zitakuwa katika albam mpya ya Beyonce lakini taarifa mpya zinaweka wazi kuwa, orodha waliyoitoa siyo sahihi na ni ya uongo
Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
Unknown
AUTHOR
14 March 2013 at 02:33 delete

Pole kwao beyonce na jigga

Reply
avatar