Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo Akutana na Watanzania Nchini Uingereza

 
Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania, Mhe. Sospeter Mhongo, akiwa Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kallaghe, akiangalia Kitabu cha wageni kilichopo Ofisini hapo, kabla ya kusaini Kitabu hicho.
Mheshimiwa Waziri Sospeter Mhongo (kulia) akiongea na baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji mapema leo kwenye Mkutano wake ambao aliufanya kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London, (kulia),Mhe. Balozi Peter Kallaghe, akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mhe. Waziri, alipokuwa akiongea na Wawekezaji hao wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta hiyo ya Nishati na Madini.
Mheshimiwa Waziri, akibadilishana mawazo na Wawakilishi kutoka Kampuni ya Margin Capital ya Uingereza, mara baada ya kumalizika mkutano na Wafanyabiashara na Wawekezaji hao.
Mheshimiwa Waziri Sospeter Mhongo (kati), akiwa kwenye picha ya pamoja Wawekezaji, (kushoto) Bwana Manubai Teraiya, mwakilishi wa Lloyds Eastern Group na (kushoto) ni Dada Gillian Raini Mwakilishi wa Kampuni ya East Africa Ventures
Waziri wa Nishati na Madini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo, yuko nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi.Mhe. Waziri amekutana na baadhi ya Wafanyabiashara na Wawekezaji wenye nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Nishati na Madini nchini Tanzania.
 
Mhe. Waziri Sospeter, alielezea hali halisi ya Uchumi iliyopo nchini, hususan kwenye sekta ya Nishati na Madini. Aidha alielezea fursa zilizopo kwa Wawekezaji wa kigeni na Wajasiliamali wa Kitanzania kuja kuwekeza nchini, ili kulipatia taifa maendeleo ya kiuchumi na kufungua ajira kwa Watanzania
Leo Jumanne tarehe 26 Februari 2013, Mheshimiwa Waziri anatarajiwa kukutana na Watanzania waishio Uingereza kuzungumzia maendeleo ya sekta ya nishati na madini Tanzania na pia kubadilishana nao mawazo kuhusu maendeleo ya sekta hiyo.
Ubalozi wa Tanzania, London unapenda kuwakaribisha watanzania wote katika Mkutano huo utakaofanyika Ubalozini (3 Stratford Place, London W1C 1AS) kuanzia saa 11 Jioni. (17.00PM)

Previous
Next Post »