Wauawa kwa kutoa chanjo ya Polio Nigeria


Ripoti kutoka nchini Nigeria zinsema kuwa watu 12 wakiwemo wafanyakazi waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio kwa watoto, wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Maafisa wa afya wameambia BBC kuwa wafanyakazi wanane waliokuwa wanatoa chanjo waliuawa mjini Kano,na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Walioshuhudia mauaji hayo wanasema kuwa, watu wengine 8 waliuawa katika kituo cha afya maeneo ya Hotoro, karibu na mji wa Kano.

Miongoni mwa waliouawa ni wanawake waliokuwa wanawasubiri watoto wao, waliokuwa wanachanjwa.

Baadhi ya viongozi wa kiisilamu, Kaskazini mwa Nigeria wamekuwa wakipinga chanjo ya Polio, wakisema inasababisha watu kukosa uwezo wa kuzaa.

Previous
Next Post »