Rais wa
Gambia Yahya Jammeh ametoa amri kuwa wafanyikazi wote wa umma
watafanya kazi siku nne pekee kwa wiki kuanzia leo Ijumaa . Ijumaa sasa itakuwa
siku ya mapumziko sawa na Jumamosi na Jumapili. Rais Jammeh anasema iwapo
wananchi wa Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki watapata muda zaidi wa
kusali, kushiriki maswala ya kijamii na kulima mashamba yao. Kwenye taarifa amesema
wananchi wa Gambia wanapaswa kurejea mashambani na kupanda chakula na
kuhakikisha wanakula chakula hicho ili taifa hilo liwe tajiri na lenye
afya.
Amesema kuwa mishahara yao
haitapunguzwa kwa sababu kwa siku hizo nne watu watafanya kazi zaidi ya saa za
kawaida ili kulipiza siku ya tano.
Shule za kitaifa
hazitafunguliwa tena siku ya ijumaa.Sekta za kibinafsi zitafanya kazi hadi
ijumaa lakini hazitaweza kufanya biashara yoyote na serikali siku
hiyo.
Rais Jammeh mwenye historia
ya kuwa na tabia za kustaajabisha, hajawapa wananchi Gambia muda wa kujiandaa
kwa mfumo huo mpya.
Mwaka 2007 alitangaza kuwa
anaweza kutibu ungonjwa wa Ukimwi kwa muda wa siku tatu akitumia mchanganyiko wa
dawa za kienyeji. Tamko hilo lililaaniwa na wataalam wa matibabu kote
duniani.
Pia amekuwa akishtumiwa kwa
ukiukaji wa haki za binadam.
Mwaka jana wafungwa tisa
waliokabiliwa na hukumu ya kifo walipigwa risasi na maafisa wa polisi huku rais
Jammeh akiapa kuwaua wafungwa wote waliohukumiwa kifo katika muda wa wiki
kadhaa. Baadaye alisimamisha mauaji hayo baada ya kukosolewa vikali na jamii ya
kimataifa.
EmoticonEmoticon