BAADHI
ya Madiwani wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani hapa
wameilalamikia kamati ya kudhibiti Ukimwi ya halmashuri hiyo kwa madai kuwa
imeshindwa kukidhi huduma ya ugawaji kondomu kwa watumishi wa
halmashauri. Imeelezwa
kwamba katika suala la utoaji wa huduma hiyo ya kondomu kwa watumishi, kamati
hiyo ikishirikiana na mratibu wa Ukimwi wa halmashauri hiyo, ilijiwekea
utaratibu wa kuweka mipira hiyo katika vyoo vya halmashauri hiyo na kwamba kila
choo huwekwa boksi moja au mbili za Salama, lakini hiyo imeonekana kutofanyika
kwa muda sasa, jambo lililowafanya madiwani hao kuhoji kwa nini imekuwa
hivyo.
Madiwani
hao walitoa hoja hiyo juzi katika uchangiaji wa taarifa ya Kamati ya Ukimwi,
kwenye kikao cha baraza la madiwani cha halmashauri hiyo,kilichofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Diwani wa Kata ya Nsalala,
Mashauri Mbembela, aliitolea uvivu kamati hiyo akisema kuwa, kumekuwa na uzembe
fulani wa kutoweka boksi hizo za Salama kwenye vyoo vya halmashauri, ambapo
utaratibu huo ulibainika wazi kwamba ulikuwa ukiwasaidia ipasavyo watumishi
wake.
Hata hivyo kauli ya diwani
huyo uliwasababisha umati mzima uliokuwemo katika kikao hicho kuangua kicheko,
kwani ilikuwa ni muda mfupi tu baada ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,
Mwalimgo Kisemba, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Ukimwi kuwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa kamati hiyo ya Ukimwi.
Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo, Anderson Kabenga, akijibia hoja hiyo aliwataka wajumbe wa kamati hiyo
kuonana na watumishi wa kitengo cha kuratibu Ukimwi katika halmashauri hiyo ili
waweze kurudisha huduma hiyo ili kunusuru afya za watumishi.
Lakini pia katika
majadiliano ya hoja hiyo, madiwani hao walihoji sababu za halmashauri hiyo
kushindwa kutoa huduma ya elimu ya Ukimwi kwa ufanisi, badala yake katika mwaka
uliomalizika ni kata 10 tu ndiyo zilipata huduma hiyo.
Habari na Na Godfrey
Kahango, Mbeya
Picha - Kwa msaada wa
mtandao
EmoticonEmoticon