Blandina Changula (amezaliwa tar. 27 Julai, 1983
mkoani Shinyanga, Tanzania.
Ni muigizaji wa vipindi vya telesheni na filamu
nchini Tanzania.
Maisha ya Mwanzo
Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya
Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya
Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule
ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo
huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam
katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo
shule ambayo alimalizia kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.
Blandina Changula anatokea kundi la Kaole Sanaa
Group, ni kundi ambalo linafahamika sana nchini Tanzania kwa kutoa nyota wengi
wa uigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota hao, wengine ni Steven Kanumba,
Vincent Kigosi ( Mr Ray ), Tea na wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa
Group
Hadi sasa ameishatoa filamu nyingi,pia ni
mmiliki wa kampuni ya kutengeneza filamu ya RJ COMPANY.
EmoticonEmoticon