Wema Sepetu (kulia) akiwa na Snura Mushi.
Uwoya akiwa na Chopa.
Kutoka kushoto:…
Wema Sepetu (kulia) akiwa na Snura Mushi.
Uwoya akiwa na Chopa.
Kutoka kushoto: Cathy, Odama na Herieth.
Snura akiwa na Esha.
Stori: Imelda Mtema, ZanzibarBAADHI ya mastaa wa kike (pichani juu) waliojitokeza kumpa ‘kampani’ msanii mwenzao, Issa Musa ‘Cloud’ kwenye uzinduzi wa filamu yake ya Toba uliofanyika katika Hoteli ya Bwawani iliyopo Zanzibar, walijikuta wakiumbuka baada ya kupigwa ‘stop’ kuingia eneo hilo wakiwa na vivazi vya ajabu.
Ishu nzima ilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo wasanii hao wa Bongo Movie walialikwa kwenye ‘event’ hiyo iliyofanyika Unguja lakini bila kujua walijiandaa kwa kuvaa mavazi yao ya kimitego.
Wakiwa hotelini kabla ya kutoka kuelekea eneo la tukio, mastaa hao wakiwemo Wema Sepetu, Irene Uwoya, Halima Yahaya ‘Davina’, Jennifer Kyaka ‘Odama’ na Snura Mushi walipigiwa simu na mwenyeji wao, Claud ambaye aliwataka wavae kiheshima siku hiyo.
“Unaambiwa baada ya simu hiyo kupigwa tukaona tumeumbuka na tulichokifanya ni kwenda madukani kuanza kutafuta madira na mabaibui, yaani sisi tulijua nako tutajiachia tu,” alisema mmoja wa wasanii hao.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kutokana na urahisi wa kupatikana kwa mavazi hayo ya Kiislam visiwani humo, haikuwa kazi nguvu kwa mastaa hao kupata nguo za heshima ambazo ziliwafanya wahudhurie ‘event’ hiyo wakiwa na muonekano tofauti.
Kwa upande wa wasanii wa kiume; Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven’ JB’, Steven Mangere ‘Nyerere’, Chiki Mchoma, Hartman Mbilinyi na Juma Chikoka, walionekana wamevalia kanzu na balaghashia hivyo kuunogesha uzinduzi huo uliohudhuriwa pia na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.Habari na picha kwa hisani ya www.globalpublishers.info
EmoticonEmoticon