polisi iringa wapewa pikipiki

polisi piki f43f0
baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa jeshi la polisi mkoa wa iringa na mkuu wa mkoa

Na Denis Mlowe- Iringa
MKUU wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma amezindua mradi wa Mkaguzi wa Tarafa wa Polisi Mkoa wa Iringa na kutaka jeshi hilo kushirikiana na wananchi katika utendaji kazi ili kufanikisha malengo yake ya kuweka mji katika hali ya amani na utulivu na kuepukana na matumizi ya nguvu na kuwa jirani zaidi na jamii kwa lengo la kupata taarifa zaidi za ulinzi shirikishi na kuwajua waharifu.

Alisema hayo wakati akizindua mradi huo ulionza kuzinduliwa rasmi kitaifa tarehe 11 mwezi wa 1 mwaka huu na Inspekta Jenarali wa Polisi Said Mwema jiji Dar es Salaam na polisi kushirikiana na wananchi katika ulinzi shirikishi kwa lengo la kuleta amani na kupunguza uhalifu katika jamii.
“Kwa kuwa wananchi wanajua matukio mengi pamoja na waharifu hamna budi kuwashirikisha na kuwa nao jirani kuweza kufanya nao kazi kuweza kuleta taarifa sahihi kwenu hivyo muwe nao jirani” alisema Ishengoma.
Aidha aliwapongeza jeshi la polisi mkoani hapa kwa kuweza kupunguza kwa kiasi kikubwa makosa makubwa ya uhalifu hadi kufikia asilimia 4.4 kwa kipindi cha mwaka 2012 na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwa mwaka huu na kumaliza kabisa makosa hayo kwa kuwatumia wakaguzi wa tarafa.
Dk Christine Ishengoma katika uzinduzi huo alikabidhi pikipiki 18 kwa maafisa wa polisi ambao ni wakaguzi wa tarafa 15 huku pikipiki tatu zikikabidhiwa kwa kikosi cha usalama barabarani aliwataka polisi mkoani hapa kuepuka kujihusha na vitendo vya uharifu akidai kufanya hivyo kunaathiri utendaji kazi kwa jeshi hilo kama baadhi ya mikoa iliyokutwa na polisi wakijihusisha na makosa ya kinidhamu na kuwasisitiza kuzitumia kwa uangalifu pikipiki hizo ziweze kudumu.
Awali akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo Mkuu wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamshina msaidizi wa Jeshi la Polisi Kamanda Michael Kamuhanda mkoani alisema kwamba lengo la mradi huo ni kupunguza uharifu kuanzia ngazi ya familia,mtaa, kitongoji, kata, tarafa, wilaya, mkoa hadi ngazi ya kitaifa ili kuimarisha maendeleo ya ustawi wa jamii.
Aidha Kamanda Kamuhanda aliongeza kwamba lengo la mpango huo ni kuunganisha kila familia katika kutambua viashiria vya uvunjifu wa amani, stadi za utatuzi wa migogoro na umuhumu wa ustawi wa jamii katika mkoa wa Iringa. “Ieleweke kwamba wamiliki halisi wa mradi huu ni wakaguzi wa tarafa na sio vinginevyo” alisema
Kamuhanda aliwataka wakaguzi wa tarafa wayatambue maeneo yao ya kazi, kuwatambua wakazi wa maeneo hayo aidha kuwatambua wadau wa polisi jamii na kushirikiana nao kwa kuandaa mpango kazi kwa kutoa elimu kwa jamii hiyo.
“Wakaguzi wa tarafa watahakikisha wanaratibu na kusimamia miradi yote ya polisi na jamii kwa kushirikiana na vitengo vingine na vikosi vyote katika maeneo yao kama madawati ya ukatili wa kijinsia, intelejensia, kampuni binafsi za ulinzi” alisema Kamuhanda“
Mkuu huyo wa jeshi la polisi mkoani hapa alitaja Kauli mbiu ya jeshi la hilo ni” Doria na misako kwanza,ushirikishwaji wananchi kwanza kazi za ofisini”
Previous
Next Post »