Polisi Dar yawashilikilia askari watano kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa Tshs. 150m. zilizoporwa eneo la Kariakoo.


Jeshi la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam inawashikilia askari polisi watano kwa tuhuma za upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 150 mara baada ya tukio la uporaji lililofanyika eneo la Kariakoo mnamo tarehe 14/12/2012.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova (pichani) amesema baada ya tukio hilo zilipatikana taarifa kuwa fedha hizo zilipotea baada ya mtuhumiwa Augustino Kayula na Frank John Mwangiba kukamatwa akiwa na bastola aina ya Browing lakini hakuwa na fedha zilizoporwa, na ambaye anasemekana ndiye aliyepora fedha hizo akiwa na wenzake.

Kamanda Kova amesema pamoja na kukamatwa kwa askari hao pia wamekamatwa majambazi wawili waliohusika na tukio hilo ambao ni ambao ni Deogratias Kimaro mkazi wa Kilakala na Kulwa Mwakabala Mkazi wa Kijiwesamli wilaya ya Ilala.

Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na gwaride la utambulisho.

Previous
Next Post »