Kagame akubali kutumwa ndege zisizo rubani DRC

Rais Paul Kagame wa Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema hana wasiwasi na pendekezo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutuma ndege zisizo na rubani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Baraza hilo linapaswa kufafanua ni kwa jinsi gani ndege hizo zitakomesha vitendo vya usalama mdogo kwenye eneo hilo. Rais Kagame ameyasema hayo kwenye kikao na waandishi wa habari mjini Kigali.
Mapema mwezi huu baraza hilo lilipendekeza kutumwa ndege zisizo na rubani mashariki mwa Kongo lakini Rwanda ililipinga pendekezo hilo ikiomba kuwepo maelezo ya kutosha juu ya azimio hilo.

Previous
Next Post »